Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salah kulipwa Sh7 milioni kwa saa Liverpool

Muktasari:

  • Mohamed Salah ameifungia Liverpool mabao 32 katika mechi 45 za mashindano tofauti msimu huu huku akipiga pasi 22 za mwisho.

Liverpool itamlipa kiasi cha Pauni 2,232 (Sh7.6 milioni) kwa saa mshambuliaji wake Mohamed Salah kupitia mkataba mpya baina yake na nyota huyo wa Misri.

Leo, Aprili 11, 2025 klabu hiyo imethibitisha kuwa Salah amesaini mkataba mpya wa miaka miwili utakaodumu hadi Juni, 2027 na kumaliza wasiwasi uliokuwepo wa nyota huyo kuondoka bure kutokana na mkataba wa mwanzo kufikia tamati Juni mwaka huu.

Katika mkataba huo mpya, Salah atalipwa kiasi cha Pauni 375,000 (Sh1.3 bilioni) kwa wiki huku akilipwa kiasi cha zaidi ya Pauni 53,571 (zaidi ya Sh182 milioni) kwa siku.

Kwa saa, nyota huyo raia wa Misri ataingiza kiasi cha Pauni 37.2 (Sh126,656).

Kiasi cha Pauni 375,000 ambacho Salah atalipwa katika mkataba mpya, ni ongezeko la Pauni 25,000 kutoka kiasi alichokuwa akipokea katika mkataba wake unaomalizika ambacho ni Pauni 350,000 kwa wiki.

Uamuzi wa Liverpool kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili Salah, umeonekana kuvunja utamaduni wa muda mrefu wa timu hiyo wa kutotoa mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja kwa mchezaji mwenye umri zaidi ya miaka 30.

Kiwango bora cha Salah mwenye umri wa miaka 32 kinaonekana kuilazimisha Liverpool kufanya hivyo ikihofia kumpoteza mfungaji wake tegemeo ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya timu hiyo tangu alipojiunga nayo mwaka 2017 akitokea AS Roma.

Katika msimu huu, Salah ameifungia Liverpool mabao 32 katika mechi 45 huku akipiga pasi za mwisho 17.

Kumuongezea mkataba Salah kunaonekana kutaishusha presha Liverpool ambayo ilikuwa na wasiwasi kuwa nyota huyo wa Misri angetimkia Saudi Arabia kwa uhamisho huru.

Mchezaji huyo amesema kuwa anajisikia furaha kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Liverpool na lengo lake ni kushinda mataji.

“Nina furaha. Tuna timu nzuri sasa. Kabla tulikuwa na timu kubwa lakini nimesaini kwa sababu nafikiria tuna nafasi ya kushinda mataji mengine na kufurahia soka langu,” amesema Salah.