Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo amchumbia rasmi Georgina

Muktasari:

  • Ronaldo anaichezea Al-Nassr ya Saudi Arabia na wanandoa hao wanaishi jijini Riyadh.

Nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo, ametangaza uchumba na mpenzi wake wa muda mrefu, Georgina Rodríguez baada ya miaka tisa ya kuwa pamoja.

Georgina, mwenye asili ya Argentina na Hispania, alithibitisha habari hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram jana Jumatatu, Agosti 11, 2025 akionesha pete ya almasi kwenye kidole chake.

“Ndiyo nakubali. Katika hili na maisha yangu yote,” aliandika kwa Kihispania.

Kabla ya hapo, Georgina alikuwa amewahi kuvalia pete nyingine ya almasi, lakini wawili hao walikuwa bado hawajachumbiana rasmi. Tetesi za uchumba zilianza mwezi uliopita baada ya Georgina kushiriki picha za chakula cha usiku chenye mandhari ya harusi, mapambo ya maua meupe na bendi ya muziki.

Mwezi uliopita, Ronaldo aliweka wazi kwa nini bado hawajafunga ndoa.

“Ninapomwambia, ‘tutakapopata hisia hiyo sahihi,’ anajua ninachomaanisha. Inaweza kuwa mwaka mmoja, miezi sita au mwezi mmoja. Nina uhakika kwa asilimia 1000 itatokea,”alisema Ronaldo.

Wawili hao wamekuwa pamoja tangu 2016 na wana binti wawili Alana (7) na Bella (2). Georgina pia ni mama wa kambo wa watoto watatu wengine wa Ronaldo.

Katika kipindi chake cha I Am Georgina kwenye Netflix, alifichua jinsi marafiki wanavyomchangamsha kwa kumuliza kila mara kuhusu tarehe ya harusi, wakirejea hata wimbo wa Jennifer Lopez “The Ring or When” kumtania.

Hata bila kufunga ndoa, Ronaldo mara kadhaa amekuwa akiishi na Georgina kama mke wake. Mwaka jana Desemba, kwenye tuzo za Globe Soccer Awards jijini Dubai, alisema: “Ni heshima kubwa kushinda tuzo hii. Mwanangu mkubwa yupo hapa, mke wangu [Georgina] yupo hapa.”

Katika michezo ya mitandaoni ya Mr. and Mrs. kwenye YouTube mwezi Agosti, wote walionekana pia wakiwa wamevaa pete za ndoa. Katika mahojiano mengine, Ronaldo alimtaja Georgina kama mke wake.

Kwa sasa, Ronaldo anaichezea Al-Nassr ya Saudi Arabia, na wanandoa hao wanaishi mjini Riyadh.