Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto wabadilisha maisha ya Ronaldo

Muktasari:

  • Ronaldo sasa anategemea kupata mtoto wanne kutoka kwa mchumba wake

Madrid, Hispania.Wakati mtoto wake wanne akitarajiwa, Cristiano Ronaldo amekiri kuwa kuwa baba kumebadilisha maisha yake kwa namna tofauti.

Watoto wa nyota huyo ni pacha Mateo na Eva na kaka yao Cristiano Jr., pia mchumba wake Georgina Rodriguez anategemea kujifunga mwezi ujao mtoto wa kike aliyepewa jina la Alana Martina.

"Kuiona familia yangu ikikuwa ni jambo linalonipa heshima ya kipekee," Ronaldo alilimbia jarida la Hola! magazine.

"Nafurahi kila dakika.

"Kuwa baba kumenifunza jinsi ya kupenda kitu nilichokuwa sijui kama kipo. Imenifanya kuwa mpole na kunipa mtazamo mwingine nini maada ya maisha."

Ronaldo alifafanua kuhusu masuala yake ya mitindo kujuishwa na  CR7 Junior Collection, pia alijadili juu ya mtoto wake kujiingiza katika masula ya mitindo.

"Cristiano Jr. anapenda masuala ya mavazi na sasa ningependa kuwa tunavaa zinazofanana," aliongeza. "Mavazi haya mapya yatatoa nafasi kwa wazazi na watoto wao kuvaa nguo zinazofanana.

"Mtoto wangu anapenda picha. Anajua kupiga pozi za kuvutia  za picha ningependa siku moja aweze kuonyesha mavazi kitu anachokipenda."