Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raundi tatu Championship Tanzania kupigwa muda mmoja

Muktasari:

  • Mtibwa Sugar inayoongoza msimamo wa Ligi ya Championship itakuwa ya kwa kupanda daraja ikiwa itaibuka na ushindi ugenini dhidi ya Bigman katika raundi ya 28.

Dar es Salaam. Katika kuhakikisha inaepuka vitendo vya upangaji matokeo katika Ligi ya Championship, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeamua mechi za raundi zote tatu zilizobakia kuchezwa muda mmoja.

Awali ratiba ya mwanzo ililazimisha mechi za raundi ya mwisho tu kuchezwa muda mmoja lakini taarifa iliyotolewa leo, Jumamosi Aprili 26, 2025, imeeleza kwamba ratiba ya mechi kuchezwa muda mmoja ni kuanzia raundi ya 28.

“Ligi ya Championship ya NBC msimu wa 2024/2025 inaingia kwenye mzunguko wa 28 leo Jumamosi Aprili 26, 2025 ambapo kila klabu imesaliwa na michezo mitatu tu kabla ya kumaliza msimu.

Bodi ilipanga na kutangaza kuwa michezo yote ya kila mzunguko uliosalia itachezwa katika tarehe na muda mmoja kwa lengo la kuongeza usawa kwenye ushindani baina ya timu shiriki.  

Kwa sababu inafahamika kuwa ushindani na msukumo umeongezeka zaidi katika kipindi hiki klabu zinafanya jitihada za kutimiza malengo yao ya msimu, Bodi imeongeza nguvu katika usimamizi wa michezo hiyo ili msukumo huo uzae burudani viwanjani badala ya kusababisha uvunjifu wa Kanuni za Ligi na sheria za mpira wa miguu,” imefafanua taarifa ya TPLB.

TPLB pia imeendelea kusisitiza kutofanyika kwa upangaji wa matokeo katika raundi hizo tatu za mwisho.

“Ni wajibu wa kila mdau wa Ligi hiyo kuhakikisha anafuata Kanuni za Ligi ikiwemo kujiepusha na kukumbusha wengine kutojihusisha na vitendo vyovyote vinavyoashiria upangaji wa matokeo.

“Bodi ya Ligi Kuu Tanzania itachukua hatua kali za kinanuni kwa kila mdau atakayebainika na kuthibitika amejihusisha kwa namna yoyote na

upangaji wa matokeo kwasababu jambo hilo ni katika mambo yanayoweza kushusha hadhi ya Ligi,” imesema taarifa hiyo.

Mechi za raundi ya 28 ambazo zitachezwa muda mmoja leo ni baina ya Cosmopolitan na Stand United, Green Warriors na Biashara United, Transit Camp na TMA, Kiluvya United dhidi ya Mbuni, Mbeya Kwanza dhidi ya Afrucan Sports, Bigman na Mtibwa Sugar, Geita Gold na Mbeya City na Songea United itacheza na Polisi Tanzania.

Mtibwa Sugar inayoongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 66, itapanda Ligi Kuu ikiwa itapata ushindi wa ugenini dhidi ya Bigman.