Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KenGold ilivyofuata nyayo za Ihefu, Mbeya Kwanza

Muktasari:

  • KenGold inashika mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na pointi 16 ilizokusanya katika mechi 27.

Dar es Salaam. KenGold jana imekuwa timu ya kwanza kushuka daraja katika Ligi Kuu msimu huu baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Matokeo hayo yameifanya KenGold ibakie na pointi zake 16 ambazo hazitoshi kuifanya ibakie kwenye ligi hata kama ikipata ushindi katika mechi zake tatu zilizobakia.

Hadithi ya KenGold inatukumbusha misimu kadhaa nyuma kwa timu ambazo zilipanda daraja na kushuka baada ya kushiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu mmoja pekee.


MBEYA KWANZA

Mbeya Kwanza iliyopanda daraja msimu wa 2021-2022, ilishindwa kushikilia bomba na kujikuta ikirudi Championship msimu huo ulipomalizika baada ya kumaliza mkiani mwa msimamo na pointi zake 25.

Wakati Mbeya Kwanza inapanda daraja msimu huo, ilimaliza kinara wa Championship kama ilivyokuwa kwa KenGold ilivyopanda 2024-2025, hivyo hadithi zao ni kama zinafanana.

Mbeya Kwanza katika msimu wao mmoja wa ligi ambapo hadi sasa wapo Championship wakipambana kurejea juu, ilicheza mechi 30, ikashinda tano, sare 10 na kupoteza 15.


GWAMBINA&IHEFU

Kabla ya hapo, msimu wa 2020-2021, Dodoma Jiji, Gwambina na Ihefu zilikuwa timu ngeni ligi kuu baada ya kupanda daraja, lakini mwisho wa msimu Gwambina na Ihefu zikarudi zilipotoka ikiiacha Dodoma Jiji hadi leo ikipeta.

Ihefu ambayo baada ya kurejea Championship msimu wa 2021-2022, ikapambana na kurudi Ligi Kuu Bara 2023-2024 kabla ya msimu huu 2024-2025 kubadilishwa jina na kuitwa Singida Black Stars inayokamata nafasi ya nne kwenye msimamo, lakini Gwambina ndiyo imepotea kabisa.


AFRICAN LYON

Timu nyingine iliyowahi kupanda daraja na kushuka msimu mmoja ni African Lyon, licha ya kwamba timu hiyo ni kama suala la kupanda na kushuka kwao ni kawaida kabla ya 2018–19 kupanda na kushuka na kushindwa kurudi tena Ligi Kuu hadi sasa.

African Lyon katika msimu huo, ilimaliza ligi na pointi 23 baada ya mechi 38, ilishinda nne, sare 11 na kupoteza 23, ikiwa ndiyo timu iliyoruhusu mabao mengi 54, pia ikifunga mabao machache 23.

KenGold pia ndiyo timu iliyoruhusu mabao mengi hadi sasa ambayo ni 50, hivyo imebakiwa na mechi tatu kupambana isiivuke rekodi ya African Lyon ya mabao 54. Hata hivyo, Singida United ndiyo timu inayoshikilia rekodi ya kuruhusu mabao mengi zaidi kwenye ligi kwa misimu ya karibuni ambayo ni 73, ilifanya hivyo msimu wa 2019-2020 iliposhuka daraja.


NJOMBE MJI

Njombe Mji nayo imefanya hivyo msimu wa 2017-2018 ilipopanda na kushuka.

Pointi 22 katika michezo 30, hazikutosha kuifanya Njombe Mji kuendelea kuwepo Ligi Kuu na hadi sasa bado haijarejea.