Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford apewa namba 14 Barcelona

Muktasari:

  • Kwa sasa, macho yote yako kwa Rashford si tu kwa uwezo wake wa kufunga na kusaidia, bali pia kwa jinsi atakavyobeba jukumu la kuvaa jezi namba 14 yenye uzito.

Marcus Rashford rasmi ni mchezaji wa Barcelona, na tayari amekabidhiwa jezi namba 14 namba yenye historia kubwa katika klabu hiyo, ikiwa ni kumbukumbu ya gwiji wa soka, Thierry Henry.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa jezi hiyo, Rashford amesema:

"Namba hii ina uzito mkubwa hapa. Ni heshima kubwa sana kupewa nafasi ya kuvaa namba aliyowahi kuvaa Thierry Henry. Najua majukumu yake na nitajitahidi kulinda heshima yake."

Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari wa Hispania, Rashford aliulizwa maswali kadhaa kuhusu maisha yake mapya, uamuzi wa kujiunga na Barcelona, na kuondoka kwake Old Trafford.

 “Sitaki kusema vibaya kuhusu Manchester United. Ni klabu iliyonilea, imenipa jukwaa la kuonyesha uwezo wangu na itanibaki kuwa sehemu muhimu ya maisha yangu. Lakini maisha huenda kwa hatua na huu ni mwanzo mpya.”

Alipoulizwa kuhusu sakata la kuachwa nje ya kikosi cha kwanza chini ya kocha Ruben Amorim kabla ya kuondoka United, Rashford hakutaka kulizungumzia kwa kina.

"Nipo mahali pazuri sasa. Sina kinyongo na mtu yeyote. Najisikia furaha, afya yangu iko vizuri na akili yangu iko hapa Barcelona," amesema kwa tabasamu.

Aliendelea kueleza kuwa amepokelewa vizuri na uongozi wa Barcelona, wachezaji wenzake na benchi la ufundi, na tayari ameanza mazungumzo ya karibu na kocha mpya, Hansi Flick, kuhusu namna ya kuendana na mfumo wa timu.

"Hii ni klabu kubwa yenye historia ya mafanikio. Naamini hapa ndiko mahali sahihi pa mimi kuendeleza ndoto yangu ya kushinda mataji makubwa," amesema Rashford.

Rashford pia aligusia jinsi ndoto za utotoni zinavyobadilika.

"Nilitimiza ndoto ya kuvaa jezi ya Manchester United. Sasa ninaandika sura mpya, jezi mpya, mji mpya – lakini ndoto ileile ya kufurahia soka,"

Kwa sasa, macho yote yako kwa Rashford si tu kwa uwezo wake wa kufunga na kusaidia, bali pia kwa jinsi atakavyobeba jukumu la kuvaa jezi namba 14 yenye uzito.