Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juventus yajitosa kwa Rashford

Muktasari:

  • Garnacho anatajwa kuwindwa na klabu kama Aston Villa, Chelsea na Tottenham, huku Sancho akihusishwa na uhamisho wa mkopo kwenda Juventus.

London, England. Hatma ya mshambuliaji Marcus Rashford ndani ya Manchester United inazidi kuwa mashakani, huku vigogo kadhaa wa soka barani Ulaya wakimnyemelea kwa karibu, ikiwemo miamba ya Italia, Juventus, ambao sasa wameingia vitani kuwania saini yake.

Rashford (28), aliyetangaza Desemba kuwa yuko tayari kwa changamoto mpya, anatajwa kuwa na nia ya kujiunga na Barcelona, ambao tayari wameripotiwa kufanya mazungumzo na wakala wake ambaye pia ni kaka yake, Dwaine Maynard.

Ingawa Barcelona wanaonekana kuwa mbele kwenye mbio hizo, taarifa mpya kutoka Sky Sport Italia zinaeleza kuwa Juventus nao wameanza kulichunguza dili hilo, wakilenga kumvuta Rashford kujiunga na kikosi chao kinachoshiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Rasford alimaliza nusu ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo ndani ya Aston Villa, ambapo alifunga mabao manne, lakini klabu hiyo ya Birmingham iliamua kutomsajili kwa mkataba wa kudumu kutokana na kiasi kikubwa cha mshahara anachopokea nyota huyo. Manchester United wako tayari kumuachia ili kuondoa mzigo wa mshahara mkubwa.

Kwa upande mwingine, kocha wa zamani wa United, Jose Mourinho, ambaye sasa yuko Fenerbahce, pia ameelezwa kuwa na nia ya kumrejesha Rashford chini ya mikono yake, huku ripoti zikidai klabu hiyo ya Uturuki iko tayari kulipa kiasi cha Pauni milioni 40(Sh140 bilioni).

Licha ya kuwa na jina kubwa katika kikosi cha United, Rashford amewekwa pembeni kwa sasa na ni miongoni mwa wachezaji watano waliotengwa huku wakitakiwa kufanya mazoezi baada ya kikosi cha kwanza kuondoka Carrington.

Rashford pia amepokonywa jezi yake namba 10, ambayo sasa imekabidhiwa kwa usajili mpya wa Pauni milioni 62.5, (Sh217 bilioni) Matheus Cunha, aliyeletwa kuziba pengo la ufungaji ndani ya kikosi cha Amorim.

Kwa sasa, anaruhusiwa kutumia uwanja wa mazoezi wa Carrington lakini tu pale ambapo kocha Ruben Amorim na kikosi cha kwanza hawapo. Uamuzi huo umechukuliwa ili kuhakikisha hakuna mchanganyiko wa wachezaji waliotengwa na wale wa kikosi rasmi.

Hata hivyo, changamoto kubwa kwa Rashford kuhamia klabu nyingine ni mshahara wake mkubwa, huku ripoti kutoka kwa mwandishi wa Hispania, Javi Miguel, zikidai kuwa mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco, bado hajaridhishwa na uwezo wa nyota huyo wa zamani wa England.

Miguel aliandika kwenye mtandao wa X: "Deco bado ni kikwazo kikuu katika mpango wa Rashford. Kuna tofauti kubwa kwenye kamati ya usajili kuhusu nani anayefaa kuongezwa kwenye safu ya ushambuliaji. Kipaumbele sasa ni kuachana na baadhi ya wachezaji ili kuondoa mzigo wa mishahara."

Wachezaji wengine waliotengwa pamoja na Rashford ni Alejandro Garnacho, Jadon Sancho, Antony na Tyrell Malacia. Garnacho anatajwa kuwindwa na klabu kama Aston Villa, Chelsea na Tottenham, huku Sancho akihusishwa na uhamisho wa mkopo kwenda Juventus, Antony akivutiwa na Real Betis, na Malacia ambaye anahusishwa kujiunga na Klabu ya Celtic ya Scottland.