Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pedro aanika udhaifu kichapo cha Al Ahly

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves amesema kilichoiponza timu yake hadi ikapoteza mchezo dhidi ya Al Ahly ugenini juzi ni makosa matatu makubwa ambayo timu yake iliyafanya.

Katika mchezo huo wa tatu katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu iliyochezwa jijini Alexandria, Misri katika Uwanja wa Borg El Arab, Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 yote yakipachikwa na Mahmoud Hassan 'Trezeguet'

Pedro alisema Yanga ilianza mchezo vizuri sana katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, licha ya kosa walilolifanya lililopelekea kuzaa bao la mapema.

Alisema kuwa katika mechi hiyo Yanga imefanya makosa makubwa matatu ambayo tayari ameshayachukua na atayafanyia kazi ili kuhakikisha hayatajirudia tena katika mchezo unaofuata, ambao utakuwa uwanja wa nyumbani.

“Siwezi kuacha kuwapongeza wachezaji ambao wamejituma sana na kiukweli najivunia sana wao kuwepo kwenye kikosi ninachokifundisha. Licha ya kupoteza, bado naiona nafasi kubwa ya uwezo wao kuisaidia timu kufanya vyema mechi zijazo.

“Siwezi kusema mechi haikuwa na makosa, yalikuwepo ndiyo maana mpinzani akapata nafasi ya kutufunga mabao mawili ndani ya dakika 90.

“Kosa la kwanza lilifanyika kipindi cha kwanza, eneo la ulinzi lililegea kidogo na wapinzani wakafanikiwa kutufunga. La pili ni kuzubaa, unaona kabisa wachezaji hawakuwa makini na kusababisha timu kuadhibiwa.

“Lakini kosa la tatu kubwa lililofanyika ni kushindwa kutumia nafasi. Tulipata nafasi nyingi ila wachezaji walishindwa kabisa kuzitumia kwa kufunga mabao,” alisema Pedro.

Yanga itarudiana na Al Ahly, Jumamosi wiki hii katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.