Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namba zaibeba Yanga kwa Pamba Jiji

Muktasari:

  • Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 55 na Pamba Jiji inashika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 22.

Yanga inakaribishwa leo na Pamba Jiji katika mechi ya mzunguko wa pili baina yao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza leo huku ikiwa na takwimu bora kulinganisha na wapinzani wao.

Timu hizo zinacheza Leo zikiwa zimekutana mara moja msimu huu na Yanga iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 ambayo yalifungwa na Ibrahim Abdullah ‘Bacca’, Stephane Aziz Ki, Kennedy Musonda na Maxi Nzengeli.

Katika kufumania nyavu, Yanga imeonesha kuwa moto wa kuotea mbali ambapo kabla ya kuingia uwanjani leo, Yanga ina wastani wa kufunga mabao 2.6 kwa mchezo.

Wastani huo wa mabao ya Yanga ya kufunga umetokana na idadi ya mabao 55 ambayo timu hiyo imepata katika mechi 21 za Ligi Kuu msimu huu.

Kwa upande wa Pamba inaikabili Yanga ikiwa haina wastani mzuri wa mabao na inashika nafasi ya pili katika chati ya timu zilizofunga idadi ndogo ya mabao katika Ligi Kuu msimu huu.

Pamba Jiji imefunga mabao 13 katika mechi 21 hadi sasa yanayoifanya iwe na wastani wa kufunga bao 0.6 kwa mchezo.

Takwimu za ulinzi ni kitu kingine kinachoiweka Yanga katika hali nzuri kisaikolojia inapokaribia kucheza mechi ya leo.

Yanga imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara tisa tu katika mechi 21 sawa na wastani wa bao 0.4 kwa mchezo wakati huo Pamba Jiji imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara 20 sawa na wastani wa bao moja kwa mchezo.

Yanga haijapoteza michezo 11 mfululizo katika ligi na katika mechi 10 zilizopita za Ligi Kuu, imepata ushindi mara tisa na kutoka sare moja.

Pamba Jiji katika mechi 10 zilizopita za Ligi Kuu, imepata ushindi mara nne, imetoka sare mbili na imefungwa nne.

Kocha wa Pamba Jiji FC, Felix Minziro amesema kuwa wanaamini mechi itakuwa ngumu lakini wanaona wanaweza kufunga Yanga.

“Hatuendi uwanjani kupoteza dhidi ya Yanga wala hatuna hofu kwa sababu ya kwenda kucheza na bingwa mtetezi kama wanavyojipanga ili kwenda juu ya msimamo na ndivyo na sisi tunavyohitaji kupata ushindi ili tujiweke sehemu nzuri kwenye msimamo,” amesema Minziro.


 ligikuu Hakuna mchezo mwepesi kwenye Ligi kuu ya

NBC, Mchezo wetu wa kesho ni moja ya mchezo mgumu kwasababu Pamba inahitaji matokeo ya ushindi ili kujiweka nafasi nzuri lakini sisi ni Yanga na ni lazima tufanye kila linalohitajika ili tushinde kesho,” amesema kocha wa Yanga, Miloud Hamdi.