Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nafasi ya Arsenal kutwaa Ubingwa yashuka baada ya kipigo cha Man United

Muktasari:

  • Hata hivyo, Arsenal bado wanaendelea kuongoza katika mbio za Ubingwa, wakitabiriwa kukusanya pointi 81.05 mwishoni mwa msimu.

Nafasi ya Arsenal kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu imepata pigo kufuatia kipigo cha mabao 3-2 ilichokipata juzi kutoka kwa Manchester United, kulingana na utabiri mpya wa supercomputer ya Opta.

Kipigo hicho kilichopatikana Uwanja wa Emirates Jumapili, kilifungwa rasmi na bao la dakika ya 87 la Matheus Cunha, na kuipa United ushindi muhimu chini ya kocha wao wa muda, Michael Carrick. Matokeo hayo yaliwanyima Arsenal nafasi ya kuongeza pengo la pointi saba kileleni mwa msimamo wa ligi.

Kwa mujibu wa Opta, kabla ya kipigo hicho, Arsenal walikuwa na nafasi ya asilimia 89.3 ya kutwaa taji lao la kwanza la Premier League tangu mwaka 2004. Hata hivyo, kufikia Jumatatu, nafasi hiyo imeshuka hadi asilimia 81.7, baada ya supercomputer kubadilisha takwimu zake kwa kutumia vigezo vya kisasa kama uwezekano wa kupata mabao (Expected goals (xG) na uwezekana wa kupata pointi (Expected points (xPTS).

Baadhi ya wachezaji wa Arsenal wakiteta jambo baada ya kichapo cha mabao 2-3 dhidi ya Man United katika mechi ya Ligi Kuu England 'EPL' iliyopigwa Jumapili, Januari 25, 2025. Picha na Mtandao

Licha ya kushuka kwa asilimia hizo, Arsenal bado wanaendelea kuongoza katika mbio za Ubingwa, wakitabiriwa kukusanya pointi 81.05 mwishoni mwa msimu. Aston Villa wanatajwa kuwa wapinzani wao wakubwa kwa sasa, wakitabiriwa kumaliza nafasi ya pili kwa pointi 73.13, wakiwazidi kwa tofauti ndogo Manchester City wanaokadiriwa kufikisha pointi 72.94.

Hata hivyo, Opta inaonyesha kuwa hata kama Aston Villa watamaliza wa pili, nafasi yao ya kutwaa ubingwa ni asilimia 9.3 pekee, huku City wakipewa nafasi ya asilimia 8.7.

Katika nafasi nne za juu, Liverpool wanatajwa kushika nafasi ya nne, licha ya kupoteza kwa Bournemouth mwishoni mwa wiki. Opta inaamini kikosi cha Arne Slot kina uwezo wa kuwapiku Chelsea, ambao wanatarajiwa kumaliza wa tano.

Kwa mujibu wa makadirio hayo, kuna uwezekano mkubwa England ikapata timu tano zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, jambo linalomaanisha Chelsea wanaweza kufuzu licha ya kumaliza nje ya nne bora.

Manchester United, licha ya mwamko wao chini ya Carrick, wanatabiriwa kumaliza nafasi ya sita, hali itakayowapeleka Ligi ya Europa. Newcastle wanatarajiwa kumaliza wa saba, wakifuatiwa na Fulham, Brentford na Everton wanaokamilisha kumi bora.

Katika mkondo wa chini wa msimamo wa ligi, Tottenham wanaendelea kukabiliwa na nyakati ngumu. Opta imetabiri Spurs kumaliza nafasi ya 15 kwa pointi 47.18, huku kukiwa na uwezekano mdogo wa asilimia 1.53 wa kushuka daraja, hali inayoongeza presha kwa kocha Thomas Frank.

Kwa upande wa kushuka daraja, Wolves wako katika hatari kubwa zaidi, wakipewa uwezekano wa asilimia 99.9 kushuka Ligi ya Championship. Burnley nao wana asilimia 97.4 ya kushuka, huku West Ham wakitajwa kuwa na uwezekano wa asilimia 81.08.

Iwapo utabiri huu utatimia, basi Wolves, Burnley na West Ham watakuwa wakazi wa Ligi ya Championship msimu ujao, isipokuwa miujiza itokee katika mechi zilizosalia.