Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mutale afunika Simba, Kibu asamehewa

Wachezaji wa Simba wakati wakifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi dhidi ya APR katika Uwanja wa Benjamin Mkapa leo Agosti 3, 2024.

Muktasari:

  • Joshua Mutale, amepokelewa kwa shangwe na mashabiki baada ya utambulisho na kupewa jezi namba saba, ambayo ilikuwa inavaliwa na Willy Onana, aliyeuzwa Uarabuni.

Dar es Salaam. Kiungo mshambuliaji wa Simba, Joshua Mutale amepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Simba baada ya utambulisho huku akiibuka na jezi namba saba ambayo ilikuwa inavaliwa na Willy Onana.

Onana anatajwa kuuzwa na Simba Uarabuni kwa dola 10,000 na kwenye utambulisho wa mastaa wapya wa Simba msimu 2024/25 jina lake halipo hivyo ni wazi sio sehemu ya kikosi cha timu hiyo.

Mutale baada ya utambulisho aliwapungia mashabiki wa timu hiyo ambao walimpokea kwa shangwe na baadaye kujiunga na wenzake hivyo kuvaa jezi yenye namba hiyo ni wazi ataitumikia msimu ujao.

Kiungo huyo amepata jezi namba ambayo alikuwa anaitumia kabla hajajiunga na Simba akiwa Power Dynamos ya Zambia.

Onana ameitumikia Simba kwa msimu mmoja alijiunga na timu hiyo msimu 2023/24 akitokea APR ya Rwanda hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo.

Mutale ndiye aliyefunika zaidi ya wachezaji wote wa zamani na wapya ambao wametambulishwa kwenye uwanja huo


Fredy atabiriwa 'top score', Kibu asamehewa

Mshambuliaji wa Simba, Fredy Michael ametabiriwa kuwa mfungaji bora Ligi Kuu Bara msimu ujao huku Kibu Denis akisamehewa na Wanamsimbazi hao baada ya sakata lake la kutojiunga na kambi nchini Misri.

Akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Simba, Ahmed Ally kwenye utambulisho wa wachezaji watakaokitumikia kikosi hicho msimu ujao alisema hakuna upinzani mchezaji huyo atachukua kiatu cha ufungaji bora.

"Haina ubishi bila shida yoyote huyu ndiye mfungaji bora msimu huu, atafunga sana Msimbazi." Alisema Ahmed

Wakati anatabiri hayo kwenye utambulisho wa Kibu alisema kama wana Simba wamemsamehe kwa kile walichokiita utovu wa nidhamu baada ya kutojiunga na kambi.

"Sisi kama mashabiki tumekusamehe, ndugu wakigombana shika jembe ukalime tumemaliza ugomvi na msimu huu bado yupo na atakuwa hapa miaka miwili.