Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni nyekundu, nyeupe kwa Mkapa

Mashabiki wa Simba wakiwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa tayari kwa tamasha lao. Picha na Simba

Muktasari:

  • Mashabiki wa Simba wanajitokeza kwa wingi kuangalia kikosi kipya cha msimu 2024/25 uwanja wa Mkapa. Yanga nao wako uwanjani kwa ajili ya kushuhudia watani wao.

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki saa nane wana Simba kushuhudia kikosi kipya cha msimu wa 2024/25 kwa Mkapa Ubaya Ubwela ni mwingi hii ni baada jezi nyekundu na nyeupe kutapakaa karibu kila kona ya nje ya uwanja.

Ni rangi za nyekundu na nyeupe ambazo zinaonekana kutawala kwa Mkapa, Simba wanaonekana kuwa tayari kushuhudia kikosi chao cha msimu mpya mapema zaidi wameanza kuingia uwanjani.

Foleni ni ndefu na mageti yote ya kuingilia mashabiki yamejaa huku utaratibu wa kuingia uwanjani ukiwa mzuri.

Kuonyesha kuwa huu ni ni Ubaya  Ubwela kama wao wanavyosema, Wanasimba wana furaha huku vikundi mbalimbali vya ushangiliaji vikionekana kuanza kazi mapema.


YANGA WAMO

Achana na nyomi ya mashabiki wa Simba waliofurika kwa Mkapa lakini mashabiki wa Yanga pia wameibuka kushuhudia watani zao.

Mashabiki wachache waliovaa jezi za Yanga za zamani na mpya wameonekana wakiingia uwanjani hapokushuhudia Mnyama akitambulisha kikosi hicho ambacho kwa asilimia kubwa ni wachezaji wapya.