Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manula atemwa Simba

Muktasari:

  • Ashi Manula, ametemwa kwenye kikosi cha Simba msimu 2024/25 baada ya kutambulishwa magolkipa wane.

Dar es Salaam. Aliyekuwa kipa namba moja wa Simba, Ashi Manula ametemwa kwenye kikosi cha timu hiyo msimu 2024/25 baada ya timu hiyo kutambulisha makipa wanne huku jina lake likiondolewa.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ndiye alikuwa anatambulisha mastaa wa kikosi hicho msimu ujao alitaja majina manne eneo la kulinda mlango ambao ni Ally Salim, Ayoub Lakred, Mohammed Camara na Hussein Abel ndio idadi ya makipa ambao wataiongoza Simba eneo la goli kipa.

Wakati wa kutaja majina hayo nyomi ya mashabiki iliyojaza uwanja wa Mkapa iliibua shangwe baada ya kusikia jina la Lakred ambaye inaelezwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita kutokana na kuumia akiwa mazoezini huko Misri.

Pia shangwe kubwa imeibuka baada ya kutajwa kwa kipa mpya wa timu hiyo ambaye amesajiliwa kwa lengo la kuziba pengo la Lakred ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa muda akiuguza jeraha alilolipata.

“Hawa ndio walinda mlango ambao tutakuwa nao msimu ujao.” Amesema Ahmed.