Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania apenya raundi ya kwanza Olimpiki

Mtanzania Thomas Mlugu (aliyevaa nguo za bluu) wakati akipambana na mpinzania wake, Tai Tin William wa Samoa kwenye Ukumbi wa Champs-De-Mars katika mashindano ya Olimpiki yanayoendelea nchini Ufaransa.

Muktasari:

  • Mwanzo mzuri kwa timu ya Tanzania kwenye michezo ya Olimpiki nchini Ufaransa baada ya Judoka Thomas Mlugu kushinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Tai Tin William wa Samoa kwa ippon.

Dar es Salaam. Umekuwa mwanzo mzuri kwa timu ya Tanzania kwenye michezo ya Olimpiki inayoendelea nchini Ufaransa baada ya Judoka Thomas Mlugu kuanza kwa ushindi mnono katika mechi yake ya kwanza ya makundi.

Mwanajudo huyo aliye kundi C amemshinda Tai Tin William wa Samoa kwa ippon katika mchezo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Champs-De-Mars.

Katika mchezo huo, Mlugu alianza kwa ushindi wa wazari 10-1 (nusu pointi) kabla ya kuendeleza ubabe kipindi cha pili kwa kupata matokeo ya ippon (KO).

Kwa matokeo hayo sasa, Mlugu ameinga hatua ya 16 bora ambayo itachezwa baadaye leo akitafuta nafasi ya kutinga robo fainali, nusu na kisha fainali ambazo zitachezwa leo.

Akizungumza na Mwananchi kutoka jijini Paris inapofanyika michezo hiyo, Mlugu amesema maandalizi na ari ya kufanya vizuri ndiyo chanzo cha matokeo hayo akisisitiza kujipanga kwa mechi ijayo.

"Nilimsoma mpinzani wangu, ubora wake na rekodi zake hazikuwa za kutisha sana, wakati nacheza naye nilipaswa nilitumia akili zaidi hadi kupata matokeo haya," amesema.

Mbali na Judoka huyo, kesho Jumanne muogeleaji Collins Saliboko atakuwa akichuana kwenye mita 100 free style.

Saliboko ameliambia gazeti ili kwamba hana hofu, amejiandaa na ndoto yake ni kufanya vizuri kwenye michezo hiyo.

Pia nyota mwingine, Sophia Latiff atachuana Ijumaa Ijayo kwenye mita 50 freestyle.

Mlugu, Saliboko na Latiff wote wanashiriki Olimpiki hiyo kupitia nafasi za upendeleo baada ya kutofuzu awali katika mashindano ya mashirikisho yao ya kimataifa.

Watanzania wengine waliofuzu Olimpiki ni wanariadha Alphonce Simbu, Gabriel Geay, Magdalena Shauri na Jackline Sakilu ambao watachuana kwenye mbio ya marathoni Julai 10 na 11 kwa wanaume na wanawake.