Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco matumaini kibao Stars, Burkina Faso walalama

Muktasari:

  • Taifa Stars inaongoza msimamo wa kundi B la Mashindano ya CHAN 2024 ikiwa na pointi tatu.

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Morocco', amesema ushindi wa kwanza wa timu hiyo wa michuano ya CHAN umetoa mwanga mkubwa wa kikosi hicho kufanya vizuri zaidi.

Kauli ya Morocco, inajiri baada ya timu hiyo kuanza vyema michuano ya CHAN kufuatia kuifunga Burkina Faso mabao 2-0, katika mechi ya kwanza ya ufunguzi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

"Narudia kusema tena mwaka huu tuna kikosi kizuri na bora ambacho naamini kinaweza kutufikisha hatua za mbali zaidi ya tunavyotarajia," amesema.

Aidha Morocco amesema licha ya jinamizi la timu hiyo kutofanya vizuri katika michuano iliyopita, ila mwaka huu utakuwa ni wa tofauti zaidi kwa sababu ya jitihada zinazoonyeshwa na wachezaji.

"Ni kweli tumekuwa tunafanya vibaya sana na tulikuwa tunaishia hatua za makundi pekee, ila nafikiri sio muda wa kuangalia hilo kwa sababu hii ni michuano mingine na isitoshe pia tupo nyumbani,"amesema.

Wakati Morocco akikoshwa na matokeo hayo, mwenzake wa Burkina Faso, Issa Balbone amesema sababu ya kichapo hicho ni kuchelewa kufika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mechi hiyo, Balbone amesema kikosi cha timu hiyo kilichelewa kufika jijini Dar es Salaam hali iliyosababisha wachezaji kushindwa kucheza vizuri zaidi.

Kocha wa Burkina Faso, Issa Balbone

"Tulifika hapa siku mbili kabla ya mechi husika, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limetuathiri kwa sababu ya kushindwa kupata muda mrefu wa kuendana na mazingira husika," amesema.

Licha ya kauli hiyo, ila Balbone alisifu ubora wa nyota wa Stars, huku eneo la kiungo likionekana kumvutia zaidi katika mechi hiyo ya ufunguzi kundi B.

"Walicheza vizuri eneo la katikati na kutunyima nafasi ya kutengeneza mashambulizi kama tulivyotarajia, siwezi kusema kucheza kwao nyumbani imewasaidia, ila nawapongeza kwa hilo," amesema.