Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mjue Buba Jammeh winga mpya Yanga

Winga mpya wa Yanga, Buba Jammeh. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Jammeh anakuwa mchezaji wa pili raia wa Gambia kusajiliwa na timu inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, wa kwanza akiwa ni Lamine Jarju aliyepo Singida Black Stars.

Dar es Salaam. Leo Jumamosi, Saa 7:00 usiku, Yanga imemtambulisha Buba Jammeh kuwa mchezaji wake mpya ikimnasa kutoka Interclube ya Angola kwa mkataba wa miaka miwili.

Mchezaji huyo ana umri wa miaka 24 na ni raia wa Gambia ingawa pia ana uraia wa Angola ambako ameishi kwa miaka mitano.

Hadi anajiunga na Yanga, Jammeh ameitumikia Interclube katika michezo saba yote ikiwa ya Ligi Kuu Angola na kufunga bao moja.

Mchezaji huyo anamudu kucheza winga za pande zote kwa vile ana uwezo wa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha akibebwa na kasi pamoja na chenga za maudhi.

Jammeh anayemudu pia kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati, ana uzito wa kilo 60 na urefu wa sentimita 177.

Jammeh anakuwa mchezaji wa pili raia wa Gambia kusajiliwa na timu inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, wa kwanza akiwa ni Lamine Jarju aliyepo Singida Black Stars.