Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi, Ronaldo nje Ballon d'Or 2024

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Katika orodha ya wachezaji 30, nyota 10 kati ya hao wanachezea Ligi Kuu England na baada ya hapo kutakuwa na mchujo wa kuwapata mastaa watatu wa mwisho ambao mmoja wao atachaguliwa katika sherehe zitakazofanyika Oktoba 28, 2024 huko Theatre du Chatelet katikati ya Jiji la Paris.

Paris, Ufaransa. Majina ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya Ballon d'Or 2024 yametajwa huku mjadala mkubwa ukiibuka juu ya nani anaweza akashinda baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kukosekana kwa mara ya kwanza katika orodha hiyo baada ya miaka 21.

Kwa upande wa wachezaji wanaocheza timu za Ligi Kuu England mastaa wa Manchester City, Rodri na Erling Haaland ndio wanapewa nafasi ya kushinda.

Rodri ambaye msimu uliopita alishinda taji la nne la Ligi Kuu England akiwa na Man City anapewa nafasi pia kwa kutokana na mchango wake katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kilichobeba ubingwa wa Kombe la Euro 2024, pia alikuwa mchezaji tegemeo katika kuifikisha timu yake kwenye fainali ya Kombe la FA ambako walipoteza dhidi ya Man United.

Katika orodha ya wachezaji 30, nyota 10 kati ya hao wanachezea Ligi Kuu England na baada ya hapo kutakuwa na mchujo wa kuwapata mastaa watatu wa mwisho ambao mmoja wao atachaguliwa katika sherehe zitakazofanyika Oktoba 28, 2024 huko Theatre du Chatelet katikati ya Jiji la Paris.

Mbali ya Rodrigo, tuzo hii inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuchukuliwa na mastaa wa Real Madrid, Vinicius Jnr na Jude Bellingham ambao wanatarajiwa kuwapo katika orodha ya mastaa watatu wa mwisho.

Vinicius na Bellingham waling'ara msimu uliopita kwa kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika kikosi cha Madrid, Dani Carvajal mwenye umri wa miaka 32 pia alichaguliwa kutokana na mafanikio aliyopata mwaka huu akishinda ubingwa Euro 2024 akiwa na timu ya taifa ya Hispania, ubingwa wa La Liga na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Madrid.

Wachezaji wengine kutoka England wanatokea Man City, Arsenal, Liverpool na Chelsea, lakini hakuna hata mmoja kutoka Manchester United.

Erling Haaland ambaye ameshinda taji la Ligi Kuu England naye anapewa nafasi kutokana na mchango wake katika utupiaji wa mabao kwenye kikosi cha Man City msimu uliopita ambapo aliibuka mfungaji bora wa EPL kwa mabao yake 27.

Mbali ya Haaland, Phil Foden ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Chama cha Wachezaji wa Soka la Kulipwa (PFA) amechaguliwa katika orodha ya mastaa wanaowania tuzo hiyo sambamba na beki Ruben Dias.

Cole Palmer ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya England katika michuano ya Euro kilichofika fainali, naye alichaguliwa akiungana na staa mwenzake wa England, Bukayo Saka.

Upande wa Arsenal wachezaji wengine watatu, Declan Rice, Martin Odegaard na William Saliba wameorodheshwa.

Staa wa Madrid, Kylian Mbappe naye yumo katika orodha hii lakini hapewi nafasi kubwa ya kusonga mbele kwa sababu hakupata mafanikio makubwa kwa mwaka huu licha ya kumaliza mfungaji bora wa Ligue 1.

Kwa upande wa wanawake nyota kadhaa wa England wamerodheshwa ikiwa ni pamoja na dada wa beki Reece James, Lauren ambaye anaichezea Chelsea.

Kwa upande wa makipa, nyanda wa Mamelodi Sundowns na timu ya taifa ya Afria Kusini, Ronwen Williams ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Afrika Kusini kuchaguliwa kuwania tuzo za Ballon d'Or.

Ronwen Williams amechaguliwa kuwa mmoja kati ya makipa 10 wanaowania tuzo ya Ballon d'Or kwa kipengele cha makipa.

Katika orodha hiyo, Williams amechaguliwa pamoja na makipa wengine bora duniani kama nyota wa Argentina Emiliano Martínez, kipa wa PSG na Italia Gianluigi Donnarumma na kipa wa Ureno Diogo Costa.

Kwa upande wa makocha bora, Xabi Alonso ambaye aliiongoza Bayer Leverkusen kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Ujerumani na Kombe la DFP Pokal, yote bila kupoteza mechi hata moja msimu mzima, amechaguliwa kuiwania tuzo hiyo akichuana na Pep Guardiola, na kocha wa timu ya taifa Hispania, Luis de la Fuente, 'Don' Carlo Ancelotti (Real Madrid), Gian Piero Gasperini (Atalanta) na kocha wa Argentina, Lionel Scaloni.

Kwa upande wa wachezaji watakao wania ni pamoja na:

Jude Bellingham (R Madrid)

Hakan Calhanoglu (Int Milan)

Dani Olmo (Barcelona)

Dani Carvajal (R Madrid)

Cole Palmer (Chelsea)

Ruben Dias (Man City)

Declan Rice (Arsenal)

Artem Dovbyk (Girona)

Rodri (Man City)

Phil Foden (Man City)

Antonio Rudiger (R Madrid)

Alejandro Grimaldo (B Leverkusen)

Bukayo Saka (Arsenal)

Erling Haaland (Man City)

William Saliba (Arsenal)

Mats Hummels (B Dortmund)

Federico Valverde (R Madrid)

Harry Kane (B Munich)

Vinicius Jnr (R Madrid)

Toni Kroos (Amestaafu)

Vitinha (PSG)

Ademola Lookman (Atalanta)

Nico Williams (Athl. Bilbao)

Emiliano Martinez (A Villa)

Florian Wirtz (B Leverkusen)

Lautaro Martinez (Int Milan)

Granit Xhaka (B Leverkusen)

Kylian Mbappe (R Madrid)

Lamine Yamal (Barcelona)

Martin Odegaard (Arsenal)