Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota waliong'ara sana bila kutwaa Ballon d’Or

Muktasari:

Tuzo hii ya Ballon d’Or ni ya juu kwa mafanikio ya mchezaji binafsi katika soka ambayo ni wachezaji wachache wamewahi kuitwaa na wengi wenye vipaji vya juu wameshindwa kuitwaa kama ilivyo kwa waigizaji wengi bora wameshindwa kutwaa tuzo ya Oscar.

 

Paris, Ufaransa

Tuzo ya Ballon d’Or hutolewa kwa wachezaji soka bora duniani kama ilivyo kwa tuzo za Oscar zinazotolewa kwa waigizaji bora na tuzo ya Nobel inayotolewa kwa wanasayansi.

Tuzo hii ya Ballon d’Or ni ya juu kwa mafanikio ya mchezaji binafsi katika soka ambayo ni wachezaji wachache wamewahi kuitwaa na wengi wenye vipaji vya juu wameshindwa kuitwaa kama ilivyo kwa waigizaji wengi bora wameshindwa kutwaa tuzo ya Oscar.

Wafuatao ni wachezaji bora waliowahi kung'ara sana, lakini hawakuwahi kutwaa tuzo ya Ballon d’Or.

 1. Diego Maradona

Kuna orodha kubwa ya wachezaji kutoka katika nchi za Brazil na Argentina ambao hawakuwahi kutwaa tuzo ya Ballon d’Or kwa sababu hawakuwahi kucheza soka katika bara la Ulaya, Pele akiwa mfano. Lakini kushindwa kwao kupata tuzo hiyo kulitokana na waandishi wa habari wa Ulaya kushindwa kusafiri mara kwa mara kwenda Santos kumuona Pele akisakata kabumbu.

Tukiachana na Pele, kwa upande wake Diego Maradona yeye alipata bahati ya kucheza soka Ulaya katika klabu ya Napoli nchini Italia na kuwapagawisha mashabiki wa soka wa nchi hiyo kwa uwezo wake mkubwa wa kukokota mpira, kufikiri kwa haraka na kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ulaya mara mbili pamoja na kombe la Uefa.

Ingawa waandishi wa habari wa Ulaya waliona maajabu ya Maradona, lakini hawakumpa tuzo hiyo kwa sababu walikuwa wakiitoa kwa wachezaji wenye asili ya Ulaya. Kwa hiyo wachezaji Michel Platini, Igor Belanov, Marco van Basten na Ruud Gullit walitwaa tuzo hiyo wakati katika kipindi hicho Maradona ndiye aliyekuwa mchezaji bora kabisa duniani.

 2. Paolo Maldini

 Akiwa ndiye beki bora katika kipindi chake, ni vigumu kuamini Paolo Maldini hakuwahi kutwaa Ballon d’Or hasa mwaka 1994 kwani akiwa na AC Milan aliiwezesha klabu hiyo kutwaa Serie A, Supercoppa Italiana, Ligi ya Mabingwa Ulaya na UEFA Super Cup, lakini hakupewa tuzo ya Ballon d’Or. Mwaka huo huo aliiongoza Italia kushika nafasi ya pili katika Fainali za Kombe la Dunia na kutangazwa kuwa mchezaji bora wa dunia na gazeti la World Soccer, lakini tuzo wa Ballon d’Or ilichukuliwa na raia wa Bulgaria, Hristo Stoichkov aliyekuwa akiichezea klabu ya Barcelona.

 3. David Beckham

 David Beckham huwezi kumfananisha na Maradona au Messi, pia huwezi kumfananisha na George Best. Hata hivyo mwaka 1999, Beckham aliiongoza Manchester United kutwaa mataji matatu ambayo ni Ligi Kuu England, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika kipindi hicho Beckham alifahamika kwa umahiri wake wa upigaji krosi na mipira iliyokufa iliyotoa mabao mengi, lakini tuzo ya Ballon d’Or ilikwenda kwa Rivaldo.

 4. Raul

 jina la Raul linafahamika sana kwa upachikaji wa mabao. Alikuwa akiingia katika eneo la penalti ni hatari na kuiwezesha klabu ya Real Madrid kufanya vizuri katika miaka ya 90 na 2000. Kwa sababu alianza kuichezea Real Madrid akiwa na miaka 17 alionekana ataendelea kutesa kwa muda mrefu na ndiyo maana hata wahusika wa Ballon d’Or walikuwa hawafikirii kumpa tuzo hiyo mapema. Raul alikuwa akifunga mabao muhimu, lakini siyo maridadi.

 Mwaka 2001 alikaribia kutwaa tuzo ya Ballon d’Or baada ya kushika nafasi ya pili na tuzo hiyo kuchukuliwa na Michael Owen. Mwaka huo Owen alifanya makubwa akiwa na klabu ya Liverpool baada ya kufunga mabao 31. Hata hivyo watu wengine waliona Owen alipewa tuzo hiyo kisiasa za soka tu kwa kuwa England ilikuwa haijawahi kutwaa tuzo hiyo tangu mwaka 1979 wakati Kevin Keegan alipoitwaa.

 5. Alessandro Del Piero

Mwaka 1996, kijana aliyekuwa na miaka 21, Alessandro Del Piero aliifungia Juventus mabao sita katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini waandishi wa habari walimpa tuzo ya Ballon d'Or raia wa Ujerumani, Matthias Sammer huku Del Piero akishindwa kuingizwa hata katika tatu bora. Mwaka 1998, Del Piero alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Italia, lakini alishindwa kutwaa tuzo ya Ballon d'Or ambayo ilichukuliwa na mchezaji mwenzake wa Juventus, Zinedine Zidane ambaye mwaka huo alitwaa ubingwa wa dunia akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa.

 6. Stefan Effenberg

 Effenberg alikuwa hana uhusiano mzuri na vyombo vya habari. Hata hivyo, licha ya kutokukubalika nje ya uwanja kwa tabia zake, ndani ya uwanja Effenberg alikuwa akitawala mchezo huku akionekana mgomvi, akiwa na dhamira, akipiga pasi ndefu makini na mashuti ya nguvu. Mwaka 2001, Effenberg aliiongoza Bayern Munich kutwaa Bundesliga na taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu mwaka 1976. Licha ya ubora wake huo, Effenberg alinyimwa tuzo ya Ballon d’Or kwani alipewa Michael Owen. Kama Effenberg angekuwa ana uhusiano mzuri na vyombo vya habari alikuwa na asilimia kubwa ya kutwaa tuzo ya Ballon d’Or.

 7. Gianluigi Buffon

Kwa muda mrefu imekuwa ni nadra kwa makipa kutwaa tuzo ya Ballon d’Or. Makipa kama Oliver Kahn na Iker Casillas walikaribia kutwaa tuzo hiyo, lakini kipa Gigi Buffon ndiye aliyekaribia zaidi mwaka 2006. Baada ya kutwaa kombe la dunia mwaka 2006 akiwa na timu ya taifa ya Italia, yeye na beki wake Fabio Cannavaro walikuwa katika nafasi mbili za juu za kuwania tuzo ya Ballon d’Or, hata hivyo Cannavaro ndiye aliyepewa tuzo hiyo. Kipa aliyewahi kutwaa tuzo ya Ballon d’Or ni Lev Yashin aliyeitwaa tuzo hiyo mwaka 1963. Hivi sasa kipa Manuel Neuer wa Bayern Munich yupo katika orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya Ballon d’Or.

8. Dennis Bergkamp

 Kama ulibahatika kumuona Bergkamp akicheza soka katika miaka ya 90 na 2000 ujue ulikuwa ukimuangalia mchezaji mwenye kipaji cha aina yake. Kwa uwezo wake wa kumiliki mpira na uwezo wake wa kufikiri haraka na kuwapangua mabeki wa timu pinzani alistahili kutwaa tuzo ya Ballon d’Or, lakini hakupewa. Kama unabisha kuhusu uwezo wa juu wa Bergkamp tazama katika YouTube. Mwaka 1993, Bergkamp alikaribia kutwaa tuzo ya Ballon d’Or baada ya kushika nafasi ya pili akiwa nyuma ya Roberto Baggio. Baada ya kucheza kwa mafanikio katika klabu ya Ajax, Bergkamp alijiunga na Inter Milan mwaka 1993, lakini akiwa Inter hakupata mafanikio kama aliyopata Ajax hivyo waandishi kumpa tuzo Baggio, lakini Bergkamp alipoenda Arsenal alirudisha makali yake ya Ajax na kupata tena mafanikio makubwa.

9. Xavi Hernandez

Bado hajastaafu kucheza soka, lakini wakati Xavi alipokuwa katika ubora wake wa hali ya juu kati ya 2008 na 2012, alikuwa ni mchezaji muhimu katika klabu bora duniani, labda tunaweza kusema ni klabu bora zaidi katika historia ya soka. Uwezo wa Xavi wa kupiga pasi na kutambua hali ya mchezo ulifanya watu wengi walioiangalia Barcelona kipindi kile kushindwa kusahau soka la hali ya juu lililokuwa likitandazwa na klabu hiyo. Hata hivyo kipindi hicho chote kilikuwa kibaya kwa Xavi kuweza kutwaa Ballon d’Or kwani ni kipindi ambacho Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wametawala kutwaa tuzo hiyo mpaka sasa.