Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yamnasa Benjamin Sesko

Manchester, England. Klabu ya Manchester United imefanikiwa kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji hatari wa Slovenia, Benjamin Sesko kutoka RB Leipzig kwa dau la pauni milioni 73.8 (Sh250 bilioni), baada ya kuipiku Newcastle United iliokuwa mbele katika mazungumzo ya awali.

Sesko (22), ambaye amekuwa akifuatiliwa na United kwa zaidi ya miaka sita, sasa amepatiwa ruhusa ya kusafiri kuelekea Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Mashetani Wekundu.

Kwa mujibu wa Daily Mail Sport, makubaliano kati ya United na Leipzig yamejumuisha kiasi cha pauni milioni 66.4 kama ada ya awali, huku pauni milioni 7.4 zikiwa ni nyongeza kwa mujibu wa mafanikio ya mchezaji.


Newcastle watoa zaidi, lakini Sesko achagua United

Ingawa Newcastle walitoa ofa ya juu zaidi kwa Leipzig, uamuzi wa mchezaji mwenyewe kutaka kujiunga na Manchester United uliamua hatma ya uhamisho huo haraka wiki hii.

United sasa inakamilisha marekebisho mkubwa ya safu yake ya ushambuliaji chini ya kocha Ruben Amorim, ambapo tayari Matheus Cunha ametua kutoka Wolves kwa pauni milioni 62.5, huku Bryan Mbeumo akisajiliwa kutoka Brentford kwa pauni milioni 71.

Sesko alifunga mabao 21 msimu uliopita katika michuano yote akiwa na Leipzig, na tangu ajiunge na klabu hiyo kutoka Red Bull Salzburg, amecheza mechi 87, akifunga mabao 39 na kutoa pasi za mabao nane.


United yapata ushindi dakika za mwisho

Katika mbio za kuwania saini ya Sesko, Newcastle walikuwa mbele, wakimwona kama mbadala wa Alexander Isak anayehusishwa na Liverpool. Tayari Liverpool walikataliwa ofa ya pauni milioni 110 (Sh372 bilioni) kwa Isak, lakini hawawezi kurudi mezani hadi Newcastle watakapopata mshambuliaji mpya.

Kwa upande wa Manchester United, walihitaji mshambuliaji wa kati baada ya kukosa saini ya Liam Delap aliyekwenda Chelsea, Hugo Ekitike ambaye alijiunga Liverpool na Viktor Gyokeres aliyetimkia Arsenal.


Hali ya Rasmus Hojlund sasa yazidi kuwa tete

Usajili wa Sesko sasa unafungua ukurasa mpya kuhusu hatma ya mshambuliaji wa Denmark, Rasmus Hojlund, ambaye huenda akawa anapatikana kwa dau la pauni milioni 30.

AC Milan inatajwa kuwania saini yake, baada ya Inter Milan kuachana naye mapema dirisha hili. Hata hivyo, Hojlund mwenyewe amesisitiza kuwa hana mpango wa kuondoka.

“Mpango wangu uko wazi ni kubaki na kupambana kupata nafasi,” alisema baada ya kufunga bao kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Bournemouth jijini Chicago.

“Ushindani ni kitu kizuri kwangu, unaniimarisha. Nipo tayari. Watu wanasahau kwamba bado mimi ni kijana nina miaka 22 tu,” aliongeza.