Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maema, Bajaber mmoja anang'oka Simba kumpisha Loemba

Muktasari:

  • Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa na Simba katika dirisha dogo la usajili ni Mahamadou Kassali, Libasse Gueye, Nickson Kibabage, Anicet Oura, Clatous Chama na Ismail Toure.

Mchezaji mmojawapo kati ya Neo Maema au Mohamed Bajaber ataonyeshwa mlango wa kutokea na Simba ili kupisha ujio wa mshambuliaji Inno Jospin Loemba aliyenaswa na Simba katika dirisha dogo la usajili linaloendelea Tanzania.

Chanzo kutoka ndani ya Simba kimefichua kuwa kati ya wawili hao, mchezaji ambaye anaonekana kuwa katika wakati mgumu zaidi ni Maema kutokana na kiwango chake kushindwa kuishawishi klabu hiyo kuendelea naye.

Lakini kwa upande mwingine, historia ya majeraha ambayo Bajaber amekuwa nayo, inaonekana kuipa wasiwasi Simba na inaweza kumuokoa Maema ikiwa benchi la ufundi litapendekeza hivyo.

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Neo Maema. Picha na Mtandao

"Maema kiwango chake hakijaturidhisha wengi lakini pia anacheza kwa mkopo hivyo sio jambo gumu kuachana naye tofauti na Bajaber. Lakini mambo yanaweza kugeuka na pnaga likamkuta Bajaber iwanpo itaonekana tatizo lake ni sugu, jambo linaloweza kumnusuru Maema," kimefichua chanzo hicho.

Hata hivyo, Meneja Habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa hajajulishwa kuhusu hilo. "Kiukweli hadi sasa sina taarifa za jambo hilo swahiba," alisema Ahmed Ally.

Ikumbukwe hadi sasa ukiondoa Loemba, wachezaji wengine wapya waliosajiliwa na Simba katika dirisha dogo la usajili ni Mahamadou Kassali, Libasse Gueye, Nickson Kibabage, Anicet Oura, Clatous Chama na Ismail Toure.

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Mohamed Bajaber. Picha na Mtandao


Kuivaa Mashujaa leo

Katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam leo kuanzia saa 10:00 jioni, Simba itaikaribisha Mashujaa FC ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakati Simba ikiingia na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mechi iliyopita ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar, Mashujaa yenyewe ilichapwa mabao 6-0 na Yanga.

Kocha wa Simba, Steve Barker alisema kuwa wamejiandaa vyema kwa mechi hiyo.

"Kuna maendeleo mazuri kwenye timu katika maeneo mengi sio tu uwanjani bali pia nje ya uwanja na hivi sasa ni muda kwetu kuwa na ufanisi ambao utatufanya kupata pointi tatu," alisema Barker.

Kocha wa Mashujaa FC, Salum Mayanga alisema kuwa timu yake itaingia kwa tahadhari kubwa katika mechi hiyo.

"Tumejaribu kufanya masahihisho ya makosa ya mchezo uliopita. Nina imani maandalizi tuliyofanya, tupo katika hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho (leo)," alisema Mayanga.

Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Azam FC wakiwa wanajifua katika Uwanja wa mazoezi. Picha na Azam FC


Azam kujiuliza kwa TRA United

Katika Uwanja wa Azam Complex, wenyeji Azam FC wataikaribisha TRA United katika mchezo uliopangwa kuanza saa 3:00 usiku.