Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Leo kitaumana tena AFCON, kina Diarra ndo basi tena

Muktasari:

  • Hata hivyo, historia inawakumbusha kuwa mara nne kati ya sita za mwisho katika robo fainali za AFCON wamepoteza, jambo linalowafanya kuwa na kibarua kizito cha kufanya.

Dar es Salaam. Jumamosi hii, macho na masikio ya mashabiki wa soka barani Afrika yataelekezwa Morocco kushuhudia Algeria ikipambana dhidi ya Nigeria na Misri ikikutana na bingwa metetezi, Ivory Coast katika mechi za mwisho za hatua ya robo fainali za AFCON 2025.

Baada ya jana, Ijumaa kushuhudiwa mechi mbili za viwango kati ya Mali dhidi ya Senegal huku Cameroon dhidi ya wenyeji, Morocco, hizi ni mechi nyingine za kibabe kutokana na historia, wachezaji nyota na takwimu zao katika michezo ya hivi karibuni.

Algeria ambaye ni bingwa wa AFCON 2019, imeshinda mechi zote tatu za awamu ya makundi, ikiwa imefungwa goli moja tu huku golini kwao akiwepo mtoto wa nyota wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa la Ufaransa,Zinedine Zidane aitwaye Luca. Kiwango chao cha kujilinda kimeonekana kwenye hatua ya 16 bora wakati wakiibuka na ushindi wa  bao 1-0 dhidi ya DR Congo, goli la dakika ya 119 la Adil Boulbina likiipeleka Algeria robo fainali.

Hata hivyo, historia inawakumbusha kuwa mara nne kati ya sita za mwisho katika robo fainali za AFCON wamepoteza, jambo linalowafanya kuwa na kibarua kizito cha kufanya.

Kocha Vladimir Petkovic amekuwa akipanga kikosi chenye uwiano mzuri katika kujilinda na kushambulia. Ismael Bennacer yupo njia panda kutumika au laa kutokana na jeraha alilopata katika mashindano hayo, wakati Jaouen Hadjam anaonekana kurejea baada ya kupona.

Anis Hadj Moussa atakosa mashindano yote kutokana na matatizo ya kiafya. Miongoni mwa wachezaji muhimu wa mashambulizi ni Riyad Mahrez, ambaye amefunga goli tatu katika mashindano haya na Boulbina aliyefunga bao la ushindi kwenye mechi ya 16 bora.

Nigeria ambao ni washindi wa AFCON mara tatu, wanakuja kwenye mechi hii wakiwa na rekodi ya kushinda mechi zote nne tangu hatua ya makundi. Victor Osimhen na Ademola Lookman wameonyesha umahiri mkubwa kwenye mashindano haya, huku Nigeria ikifunga goli 12 na kuruhusu mabao manne tu. 

Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Msumbiji katika hatua ya 16 bora unaonyesha nguvu yao ya ushambuliaji, ingawa mechi hiyo ilihusisha tukio dogo la ugomvi kati ya wachezaji hao ambapo hata hivyo walionekana wakicheza baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mchezo huo.

Rekodi za Nigeria dhidi ya Algeria si nzuri, wamepoteza katika mechi zao nne za mwisho, ikiwemo fainali ya AFCON 2019 na mechi mbili za kirafiki, hivyo kocha wa Nigeria, Eric Chelle atakuwa na kibarua kizito cha kufuta uteja huo huku Algeria ikihitaji kuendeleza ubabe wake.

Katika mechi ya robo fainali ya mwisho, Misri ikiwa na Mohamed Salah inakutana dhidi ya Ivory Coast. Misri iliichapa Benin 3-1 baada ya muda wa nyongeza, licha ya changamoto ambayo walikumbana nayo katika mchezo huo. Ushindi huo umeongeza rekodi yao ya kutopoteza dhidi ya timu za Afrika katika mechi 14 mfululizo, wameshinda 12 na sare mbili.

Ivory Coast ilitinga robo fainali kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Burkina Faso, mabao ya Amad Diallo, Yan Diomande na Bazoumana Toure dakika za mwisho za mechi yalitosha kuwafanya kutinga hatua hii.

Elephants itashuka dimbani katika mechi hii ya robo fainali ikiwa na rekodi nzuri ya kutoshindwa katika mechi zao nne za hivi karibuni za AFCON, jambo linalowaongeza morali katika kikosi chao.

Misri inakosa wachezaji muhimu Mahmoud Trezeguet Hassan, aliyeumia katika mechi ya Benin na Mohamed Hamdy ambaye naye ni majeruhi. Hata hivyo, kocha Hossam Hassan ana machaguo mengi kwenye kikosi chake.

Ivory Coast itakosa huduma ya Christ Inao Oulai kutokana na kadi za njano alizoonyeshwa, lakini bado wana wachezaji wenye uwezo mkubwa kama Amad Diallo, aliyefunga goli tatu katika mashindano haya. Uwepo wake unatoa nguvu katika safu ya mashambuliji ya timu hiyo.