Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMC yaipiga mkwara Simba, kocha ashtuka

Muktasari:

  • Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na pointi 66 wakati huo KMC inashika nafasi ya 11 ikiwa imekusanya pointi 30.

Dar es Salaam. Benchi la ufundi la KMC limeitisha Simba kuwa isitarajie mteremko katika mechi ya Ligi Kuu baina yao itakayochezwa kesho Jumapili, Mei 11, 2025 katika Uwanja wa KMC Complex likitamba kuwa litawapa mshangao kwa kupata matokeo mazuri dhidi yao.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa kuanzia saa 10:00 jioni uwanjani hapo na kaimu kocha mkuu wa KMC, Adam Mbwana amesema kuwa hawana cha kuhofia mbele ya Simba kwa vile wanawafahamu vilivyo.

Mbwana amesema kuwa huo ni mchezo wa mwisho kwao kucheza uwanja wa nyumbani hivyo ni lazima wautumie vizuri kupata matokeo ya ushindi ambayo yatawaweka katika mahali salama kwenye msimamo wa ligi.

"KMC tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Simba. Maandalizi yote yako sawasawa. Tumepata siku kadhaa za kufanya mazoezi na kufanya tathmini mechi ya Simba na bahati tuliona mechi yao ilivyopita hivyo tuko sawa na tayari kwa mchezo.

"Tuna michezo minne kabla hatujamaliza ligi na mchezo wa kwanza ni huo dhidi ya Simba. Sisi tunakwenda kutafuta pointi tatu kwenye huo mchezo kwa sababu sisi wote tunafahamu yote ni michezo migumu, ukiacha huu wa Simba tuna michezo mitatu ugenini  inayofuata kwa hiyo huu ndio mchezo pekee uliobaki nyumbani.

"Tutajaribu kila namna na kila mbinu kutumia madhaifu ya Simba. Ni timu nzuri, timu kubwa lakini kama timu wana uimara na udhaifu wao hivyo tunachotakiwa kufanya ni kutumia huo udhaifu walionao tuweze kupata matokeo," amesema Mbwana.

Kwa upande wa Simba, kocha msaidizi, Selemani Matola amesema kuwa wanafahamu KMC wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na shauku kubwa ya kupata matokeo mazuri lakini wao wamejipanga kuhakikisha hawaangushi pointi.

Matola amesema kuwa kikosi chao kipo kamili na wao benchi la ufundi wana wigo mpana wa uteuzi wa kikosi ukizingatia wanakabiliwa na ratiba ngumu katika siku za hivi karibuni.

"Tuna ratiba ngumu, ndani ya siku 10 mechi nne lakini Allihamdullah tumeshamaliza tatu na tumebakiza moja ambayo ni mechi ya KMC. Siku zote nasema kwamba Simba hatuna mechi rahisi. Mechi zote kwetu ni ngumu lakini tunatambua ugumu wa mechi zote ambazo ziko mbele yetu sisi kwa hiyo tunahakikisha tunapambana na mechi hizi tupate matokeo.

"Wachezaji wote wako kambini na mchezaji mmoja tu ndiye majeruhi ambaye ni Mzamiru Yassin ambaye hayuko kwenye kikosi. Uwepo wa wachezaji wetu kuwa vizuri wote kambini inatupa picha nzuri katika mchezo wa kesho kuweza kufanya vizuri na kutoka na alama tatu ambazo ni muhimu kwetu sisi.

"Watu watarajie mchezo mgumu sana kwa sababu tupo katika dimba la KMC nyumbani kwao ambako Simba tuko ugenini. KMC hana matokeo mazuri lakini ana timu nzuri sana. Hawapo katika nafasi ambayo sio nzuri hivyo naamini kwamba  hawatokubali kupoteza mchezo wa kesho lakini pamoja na ugumu wao na  nyumbani kwao tumejiandaa kuhakikisha tutapata matokeo mazuri katika mchezo wa kesho," amesema Matola.

KMC inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza kwa mabao 4-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Simba iliyochezwa katika uwanja huohuo, Novemba 6 mwaka jana.

Simba wana rekodi nzuri ya ubabe dhidi ya KMC kwenye Ligi Kuu kwani hawajawahi kupoteza mechi yoyote kati ya 13 ambazo zimekutanisha timu hizo mbili.

Katika mechi hizo 13, Simba imepata ushindi katika michezo 11 na michezo miwili ilimalizika kwa matokeo ya sare.