Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kenya yang’ara , yaaibika China

Julius Yego wa Kenya akishangilia baada ya kushinda medali ya dhahabu ya kurusha mkuki mwaka jana mjini Glasgow, Scotland kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola.   Ameshinda pia medali kama hiyo nchiin China.  Picha ya Maktaba

Muktasari:

Kulingana na Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF), Kenya inashika nafasi ya juu ikiwa na medali 11, zikiwamo sita za dhahabu, ikiwamo ya Julius Yego aliyerusha mkuki, umbali wa mita 92.72.

Beijing, China. Licha ya kuongoza kwenye idadi ya medali kwenye mashindano ya ubingwa wa  dunia wa riadha yanayoendelea China, Kenya imepata aibu nyingine baada ya wanariadha wake wawili kufungiwa kwa madai ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu ya misuli.

Wanariadha hao, Joyce Zakary mwenye umri wa miaka 29 na chipukizi Koki Manunga mwenye miaka 21 walitiwa hatiani baada ya kupimwa kwenye hoteli ambako timu ya Kenya imefikia.

Kulingana na Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF), Kenya inashika nafasi ya juu ikiwa na medali 11, zikiwamo sita za dhahabu, ikiwamo ya Julius Yego aliyerusha mkuki, umbali wa mita 92.72.

Katika orodha hiyo, Kenya inafuatiwa na Marekani yenye medali 12, ingawa ina dhahabu tatu.

IAAF ilieleza kuwa Joyce Zakary, 29,  Koki Manunga, 21, wamekubali uamuzi wa awali wa kufungiwa kwao. Washiriki hao wa mbio za 400  na  mita 400 kuruka viunzi walipimwa Agosti 20 na 21 .

Joyce Zakary aliweka rekodi ya Kenya ya mbio hizo kwa muda wa sekunde 50.71  kwenye mbio za mchujo mita 400.

Manunga alimaliza kwenye nafasi ya sita katika mbio za mita 400 kuruka viunzi kwa muda wa sekunde 58.96.

Tayari, Shirikisho la Riadha  Kenya (AK) limekutana na  IAAF  na wanariadha hao wawili na limeanza uchunguzi ambako hatua stahiki zitachukuliwa nchini Kenya.

Hadi sasa,  Kenya inao wanariadha 13 wanaotumikia adhabu kwa makosa ya kutumia dawa za kuongeza nguvu misuli.

Mapema mwezi huu, Wakala wa Kupambana na Dawa za Kulevya  (WADA) ulieleza  azma ya kuanza uchunguzi haraka wa ongezeko la wanariadha wanaotumia dawa  hizo.