Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Henderson kurejea England msimu ujao

Muktasari:

  • Iwapo ataondoka kabla ya Julai 15, vilabu vya EPL vina nafasi kubwa ya kuinasa saini yake bure.

Nahodha wa zamani wa Liverpool, Jordan Henderson, anawindwa vikali na klabu ya Nottingham Forest ya England pamoja na Olympique Marseille ya Ufaransa, huku mkataba wake na Ajax ukiwa na kipengele kitakachomruhusu kuondoka bure kabla ya mwezi Julai.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na mchezaji huyo, Henderson anaweza kujiondoa Ajax kama mchezaji huru kutokana na kipengele maalum kilicho kwenye mkataba wake hatua ambayo imevutia vilabu kadhaa barani Ulaya.

Forest ni miongoni mwa klabu kadhaa za EPL zinazomfuatilia kwa karibu, sambamba na Marseille na timu nyingine kadhaa kutoka bara la Ulaya ambazo zinalenga kuimarisha safu ya kiungo kwa msimu ujao.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye alitua Ajax Januari 2024 akitokea Al Ettifaq ya Saudi Arabia, amecheza mechi 57 tangu ajiunge na miamba hao wa Uholanzi na hata kuaminiwa kwa kupewa unahodha wa kikosi hicho. Msimu uliopita pekee, alicheza mechi 45, na alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Francesco Farioli kilichokaribia kutwaa taji la Eredivisie lakini kikaporomoka dakika za lala salama.

Henderson kwa sasa bado hajafanya uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wake, huku akitathmini kama ni busara kusalia Ajax au kurudi England ili kuongeza nafasi ya kuitwa tena kwenye timu ya taifa.

Kiungo huyo bado anabaki kuwa chaguo linaloaminika kwa kocha mpya wa England, Thomas Tuchel, ambaye tayari amemjumuisha kwenye vikosi viwili vya awali tangu achukue mikoba kutoka kwa Gareth Southgate. Henderson anapigania kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki Kombe la Dunia la 2026.

Akiwa ameichezea England mara 83, Henderson ana uzoefu mkubwa kimataifa, huku historia yake ya mafanikio akiwa Liverpool ikimfanya kuwa lulu sokoni. Alicheza mechi 492 ndani ya miaka 12 akiwa Anfield, akitwaa mataji mbalimbali ikiwemo: Ligi Kuu England (2020), Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia la Klabu, FA Cup, EFL Cup, UEFA Super Cup na Community Shield.

Kwa sasa, kocha mpya wa Ajax, John Heitinga, ambaye aliwahi kuwa msaidizi wa Liverpool, anaonekana kutaka kuendelea kumtumia Henderson, lakini huenda ikawa vigumu kwa nyota huyo kusalia kutokana na kuhitaji kurudi England.

Iwapo ataamua kuondoka kabla ya Julai 15, vilabu vya EPL vina nafasi kubwa ya kuinasa saini yake bure jambo linalowafanya Nottingham Forest kuwa macho zaidi.