Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawakuachi! Hii ndiyo first eleven Simba, Yanga

Hawakuachi! Hii ndiyo first eleven Simba, Yanga

Muktasari:

  • KWANI wao wanasemaje? Ndio usemi unaotumika huko mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kuelekea mchezo wa watani wa jadi kati ya Wekundu wa Msimbazi, Simba dhidi ya Wananchi, Yanga unaotarajiwa kuchezwa leo Jumamosi kwa Mkapa.

KWANI wao wanasemaje? Ndio usemi unaotumika huko mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kuelekea mchezo wa watani wa jadi kati ya Wekundu wa Msimbazi, Simba dhidi ya Wananchi, Yanga unaotarajiwa kuchezwa leo Jumamosi kwa Mkapa.

Hakuna upande uliokaa kinyonge, amshaamsha ya tambo za hapa na pale zimeshika kasi na hiki ndio kipindi ambacho mashabiki wa Simba na Yanga huwa kuna majina ambayo wamekuwa wakiyataja midomoni mwao ili kuwatisha wapinzani wao. Patamu hapo.

Utawaambia nini mashabiki wa Simba kwa Clatous Chama, Luis Miquissone, John Bocco na Bernard Morrison na Yanga kuhusu, Yacouba Sogne, Mukoko Tonombe, Feisal Salum na Tuisila Kisinda mbona patachimbika kwa Mkapa kutokana na ubora wa wachezaji hao.

Kulingana na ubora wa timu zote mbili hiki hapa kikosi cha pamoja tulichokiunda kwa mfumo wa 4-2-3-1 kati ya Simba dhidi ya Yanga na kwa kiasi kikubwa wachezaji hawa wana nafasi kwenye vikosi vyao kuamua matokeo.

AISHI MANULA

Uwezo wa kipa wa Simba, Manula ni wazi kuwa umekuwa ukiibeba timu hiyo kuanzia kwenye Ligi ya Mabingwa ambapo waliishia hatua ya robo fainali, Kombe la FA na hata kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara na hakuna shaka kwamba anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Didier Gomes dhidi ya Yanga.

SHOMARI KAPOMBE

Anatajwa kuwa mmoja wa mabeki bora wa kulia, anauwezo wa kucheza kisasa kwa maana ya kuzuia na kushambulia, sina maana kwamba Kibwana Shomary wa Yanga hana sifa hizo, hapana lakini anaonekana kuzidiwa ubora na Kapombe ambaye aliwahi kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa Ufaransa kwenye klabu ya Cannes kabla ya kuamua kurejea nyumbani, Tanzania.

MOHAMMED HUSSEIN

Amekuwa muhimili mkubwa kwa Simba upande wa beki ya kushoto, anasifa kama za Kapombe ni mzuri kuzuia na kushambulia, kwa Yanga aliyekuwa anaonekana kuja vizuri alikuwa ni Yassin Mustapha ambaye kwa sasa ndio anarejea kikosini akitoka majeruhi, Saleh Adeyum ni mzuri kuzuia.

JOASH ONYANGO

Mkenya huyu ndiye beki wa kati wa Simba ambaye anaonekana kucheza michezo mingi zaidi ya Ligi Kuu Bara, mwanzoni mwa msimu alikuwa akicheza pacha sambamba na Pascal Wawa lakini kuna kipindi alikuwa akicheza na Erasto Nyoni au Kennedy Juma. Kwasasa anaonekana kuwa na muunganiko mzuri na Wawa, vutasa hao wameifanya Simba kuwa na ukuta imara.

PASCAL WAWA

Licha ya kwamba kasi yake imepungua kutokana na umri kumtupa mkono bado Wawa ambaye ni raia wa Ivory Coast anabaki kuwa mmoja wa mabeki bora wa kati, ni mjanja na mzoefu na uwezo wa kukabiliana na mshambuliaji yeyote, bado anaonekana kuwa sawa kiushindani.


MUKOKO TONOMBE

Huyu ni mtu na nusu akiwa sawa unaweza kumwona kila sehemu, anauwezo wa kukata umeme, unaweza kuona viungo wa Yanga wakipoteana lakini sio Mukoko, anaingia kwenye kikosi chetu kwanini? mbali na kuwa na uwezo wa kutekeleza jukumu lake la kwanza kama kiungo mkabaji (kuzuia) lakini pia anauwezo wa kusukuma mashambulizi na hata kufunga mabao.


TADDEO LWANGA

Mukoko na Taddeo Lwanga ndio viungo pacha wakabaji kwenye mfumo wetu wa 4-2-3-1, kama ambavyo amekuwa akishuhudiwa akicheza akiwa na kikosi chake cha wekundu wa Msimbazi, Mganda huyu ni mzuri mno kukata umeme hivyo atakuwa na jukumu la kuwahakikishia usalama kwa Manula na mabeki wake wanne, Kapombe, Tshabalala, Onyango na Wawa.

CLATOUS CHAMA

Mzambia huyu balaa lake ni zito, anaongoza kwenye orodha ya watengeneza mabao akiwa na asisti 13, Chama ni kati ya wachezaji hatari zaidi kwa Simba ambao Yanga wanapaswa kuwa nao makini kwenye mchezo wa dabi, anaweza kucheza kama namba 10 au winga wa kulia au kushoto.

FEISAL SALUM

Siku hizi anatumika juu, hatumiki kama kiungo mkabaji ndio maana anaonekana kutengeneza nafasi na hata kufunga, Feisal kwa kiwango ambacho alikionyesha kwenye michezo michezo miwili iliyopita dhidi ya JKT Tanzania na Ruvu Shooting anaingia kwenye kikosi chetu na kuwa kati ya viungo watatu ambao wanacheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho.

LUIS MIQUISSONE

Konde Boy ni mjanja kwelikweli Azam wanamkumbuka vizuri jinsi alivyowafanya kitu mbaya kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA, aliukata mpira akiwa kwenye mazingira magumu kwa guu lake la kushoto na kuifanya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Ruvuma.

JOHN BOCCO

Ndiye kiongozi wa Simba kwenye safu yao ya ushambuliaji, kinachombeba mbele ya Meddie Kagere na kuingia kwenye kikosi hiki licha ya kwamba wote wamepachika mabo 14 ni uwezo wa kusimama mwenyewe na akafanya mambo kama mshambuliaji wa mwisho, mbali na sifa hiyo pia anauwezo kukaba kuanzia juu na kushuka chini kutafuta mipira.