Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Grealish kukamilisha uhamisho Everton

Muktasari:

  • Mechi yake ya mwisho kuvaa jezi ya England ilikuwa Septemba mwaka jana chini ya kocha wa muda Lee Carsley.

Winga wa Manchester City, Jack Grealish, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa afya leo Jumatatu kabla ya kujiunga na Everton kwa mkopo wa msimu mzima, baada ya pande hizo mbili kufikia makubaliano.

Grealish (29) amekuwa akitarajiwa kuondoka City majira haya ya kiangazi, hasa baada ya kutolewa kwenye kikosi cha Pep Guardiola kilichoshiriki Kombe la Dunia la Klabu la FIFA. Everton imekuwa kinara wa mbio za kumsajili nyota huyo wa England, ambaye anaripotiwa kulipwa paundi laki tatu kwa wiki.

Msimu uliopita, Grealish alicheza mechi 32 kwenye mashindano yote huku akianza michezo saba pekee ya Ligi Kuu. Tangu kujiunga na City akitokea Aston Villa kwa ada ya rekodi England ya paundi milioni 100 (Sh338 bilioni) mwaka 2021, ameichezea klabu hiyo mara 157, akifunga mabao 17 na kutoa pasi za mabao 23.

Amefanikiwa kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA, na pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichonyakua mataji ya UEFA Super Cup na Kombe la Dunia la Klabu. Mchango wake mkubwa ulionekana msimu wa 2022/23 wakati City walipotwaa mataji makuu matatu (treble).

Guardiola mapema mwaka huu alimtaka Grealish kurejesha kiwango chake cha msimu wa 2022/2023, akisisitiza kuwa hana shaka na ubora wa mchezaji huyo, lakini anahitaji kupigania namba kila siku.

Kocha wa Everton, David Moyes, ambaye amesisitiza usajili wa Grealish, aliwahi kumsifu nyota huyo mwaka 2021 alipokuwa Aston Villa, akimwita mchezaji bora zaidi wa Ligi Kuu England.

Usajili huu unatarajiwa kuwa pigo tamu kwa mashabiki wa Everton, klabu inayohamia uwanja mpya wa Hill Dickinson wenye uwezo wa kubeba mashabiki 52,769 huko Bramley Moore Dock.

Grealish, ambaye amekosa nafasi kwenye kikosi cha England chini ya Thomas Tuchel, anatarajia kutumia uhamisho huu kuimarisha nafasi yake ya kurejea timu ya taifa kuelekea Kombe la Dunia la 2026 nchini Marekani, Canada na Mexico. Hadi sasa ana jumla ya michezo 39 ya kimataifa, huku mechi yake ya mwisho kuvaa jezi ya England ilikuwa Septemba mwaka jana chini ya kocha wa muda Lee Carsley.