Gamondi atajwa Singida Black Stars

Muktasari:
- Gamondi ni mmoja Kati ya makocha ambao walipata mafanikio akiwa na Yanga
Kuna taarifa za aliyewahi kuwa kocha wa Yanga, Miguel Gamondi yupo mbioni kujiunga na Singida Black Stars kuifundisha msimu ujao.
Gamondi ambaye alijiunga na Yanga Julai 11, 2023/24 akachukua ubingwa wa Ligi Kuu na FA, aliondoka Novemba 15, 2024, inaelezwa sababu ya kujiunga na Singida Black Stars ni kutokana na uzoefu wake inaoamini utaisaidia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).
Kama uongozi ukifanikiwa kupata saini yake ataziba pengo la David Ouma aliyeisaidia timu hiyo kufika fainali ya Kombe la FA na kumaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Chanzo cha ndani kutoka timu hiyo kimesema:"Gamondi alikuwa anahitajika kwa muda mrefu SBS, lakini akachukuliwa Patrick Aussems aliyewahi kuifundisha Simba kwa mafanikio...hatukuweza kumaliza naye msimu.
"Tumefikia hatua nzuri katika mazungumzo yetu (na Gamondi), muda wowote anaweza akasaini kwa ajili ya kuifundisha timu msimu ujao, ni kocha mzuri tunategemea atatusaidia sana katika michuano ya CAF."
Mwisho.