Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukocha Ligi Kuu Bara sio rahisi

Muktasari:

  • Tabora ndio timu inayoongoza kwa kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi msimu huu.

Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 unaelekea ukingoni na zimebaki raundi mbili tu ili ufikie tamati.

Ukiachana na matokeo ya uwanjani, jambo ambalo hapana shaka linaufanya msimu huu kuwa wa kipekee kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ni mabadiliko mengi ambayo yamefanyika katika mabenchi ya ufundi ya idadi kubwa ya timu zinazoshiriki ligi hiyo.

Ni timu tatu tu kati ya 16 ambazo zimefanikiwa kumaliza msimu zikiwa na makocha wakuu ambao zilianza nao huku nyingine 13 zilizobakia zikiwa zimebadilisha makocha tena nyingine zikifanya hivyo mara moja au zaidi.

Makocha ambao hadi sasa wapo katika timu ambazo walianza nazo msimu ni Fadlu Davids wa Simba, Ahmad Ally wa JKT Tanzaniana Mecky Maxime anayeinoa Dodoma Jiji.

Katika orodha ya timu vinara kwa kubadilisha makocha wakuu, Yanga, Tabora United na Kagera Sugar zimeonekana kuwa hazishikiki kulinganisha na nyinginezo.

Yanga ilianza msimu ikiwa na kocha mkuu Miguel Gamondi kisha ikanolewa na Sead Ramovic na baadaye ikampa jukumu Miloud Hamdi ingawa ipo mechi moja ambayo benchi lake la ufundi liliongozwa na kocha msaidizi Abdihamid Moalin.

Na kama tetesi zilizoibuka kuwa itaachana na Hamdi mwishoni mwa msimu huu ni sahihi, maana yake Yanga itakuwa imefundishwa na makocha wanne wakuu ndani ya msimu mmoja, idadi ya makocha ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kuifundisha timu hiyo ndani ya msimu mmoja.

Kagera Sugar yenyewe ilianza na kocha Paul Nkata na baadaye ikanolewa na Melis Medo kisha ikawa chini ya kipa na kocha wake msaidizi wa zamani, Juma Kaseja.

Tabora ndio timu inayoongoza kwa kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi msimu huu ambapo ilianza msimu ikiwa na kocha mkuu Francis Kimanzi ambaye aliondoka na nafasi yake ikachukuliwa na Anicet Kiazmak kisha akafuata Genesis Mangombe na sasa timu hiyo ipo chini ya kocha Simonda Kaunda.

Kiujumla ndani ya msimu huu tumeshuhudia timu 13 zikifundishwa na makocha wakuu 36 tofauti jambo ambalo kiuhalisia sio la kawaida na hatukuwahi kuliona kwenye ligi yetu hapo nyuma japo timu zilikuwa zikifanya mabadiliko ya mabechi ya ufundi.

Kwa wastani maana yake timu hizo 13 kila moja inakadiriwa kufundishwa na makocha watatu ndani ya msimu mmoja.

Hili halipaswi kuchukuliwa kwa hali ya kawaida na hapana shaka kuna udhaifu mahali fulani ambao unapaswa kutafutiwa tiba ili kuusaidia mpira wetu na Ligi kiujumla.

Haitakiwi kuwa sifa kuona ndani ya msimu mmoja timu inafundishwa na makocha wawili au zaidi kwani inaleta athari za kimbinu kwa wachezaji kwa vile makocha hao kila mmoja ana falsafa na mbinu zake ambazo zinamtofautisha na mwingine.

Falsafa na mbinu hizo zinahitaji muda usiopungua miezi mitatu ili ziweze kuingia vichwani mwa wachezaji na kisha waanze kufanyia kazi kwa vitendo uwanjani na ndio maana wabobezi wa masuala ya mpira wa miguu huwa hawashauri mabadiliko ya benchi la ufundi wakati msimu unaendelea.

Baadhi ya timu zinaweza kujificha katika kichaka cha utetezi kuwa zimeendelea kufanya vizuri au zimeanza kupata matokeo ya kuridhisha baada ya kubadilisha makocha lakini  kiuhalisia madhara yake huwa ni makubwa na hugusa timu nyingi na idadi kubwa ya wachezaji na hata mengine huonekana baadaye kwa timu hizo ambazo zinaona hazikukosea kubadilisha mabenchi ya ufundi kwa vile tu inaonyesha muelekeo.

Ziko sababu tofauti ambazo zinaweza kupelekea timu zifanye mabadiliko ya mabenchi yao ya ufundi ambapo kuna zile za lazima na zisizo na ulazima.

Sababu za ulazima ni kama timu kuwa na mwenendo mbaya huku ikiwa haionyeshi ishara za kubadilika na kurudi kwenye mstari na nyingine ni kutokuwa na mahusiano mazuri kati ya kocha na wachezaji jambo ambalo husababisha kupotea kwa imani baina ya pande hizo mbili, kila moja kwa mwenzake.

Mfano wa sababu zisizo za ulazima ni kocha kuonyesha misimamo ya kutotaka kuingiliwa ktika majukumu yake lakini pia hata timu kuangusha pointi katika mechi chache hali inayopelekea mihemko kwa viongozi na kufanya uamuzi kama huo.

Kwa bahati mbaya makocha wengi wanatengeneza urahisi wa kuonyeshwa milango ya kutokea na viongozi kwa vile wanakubali mikataba ambayo haina vipengele vingi vya kuwalinda na badala yake ina mianya ya kuzipa wepesi timu kuachana nao pale zinapoamua kufanya hivyo.

Lakini kama kutakuwa na vipengele vigumu vya kuvunja mikataba ya makocha, klabu zitakuwa na adabu katika ufanyaji wa maamuzi kuhusu mabenchi yao ya ufundi na hazitokuwa zinakurupuka katika utoaji hatima za makocha wao