Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FIFA yaitoza Israel mamilioni kisa Palestina

Muktasari:

  • Kanuni ya 15 ya nidhamu ya FIFA inakataza vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji wa rangi katika mchezo wa mpira wa miguu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (FIFA) limeipa Israel adhabu ya faini kiasi cha Sh491 milioni kutokana kujihusisha na kukiuka kanuni za nidhamu za shirikisho hilo.

Adhabu hiyo imetangazwa Alhamisi, Machi 19, 2026 ambapo imeenda sambamba na onyo kali kwa Israel huku ikitakiwa kuhakikisha hairudii makosa yaliyosababisha ipewe adhabu.

Uamuzi huo unafuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Palestina katika Mkutano Mkuu wa 74 wa FIFA uliofanyika Bangkok, Thailand, 2024 ikituhumu Israel kwa uvunjaji wa kanuni za nidhamu za FIFA.

Katika malalamiko hayo, Palestina iliituhumu Israel kwa  muendelezo wa vitendo vya unyanyasaji na ubaguzi wa rangi kwa Wapalestina na kutumia kauli za uchochezi pamoja na kukiuka misingi ya uungwana.

Makosa hayo ni uvunjaji wa kanuni ya 13 na 15 za nidhamu za FIFA ambazo zinakataza vitendo husika katika soka, jambo lililopelekea Israel ipewe adhabu hiyo.

Mbali na faini ya Faranga za Switzerland 150,000 (Sh491 milioni) ambayo FIFA imeitoza Israel, nchi hiyo pia imepewa onyo kali kwa vitendo hivyo huku pia ikiagizwa kuhakikisha hairudii makosa hayo.

Shirikisho la Soka la Israel limeamriwa kuonyesha katika mechi zake tatu zijazo za mashindano ya FIFA, zitakazochezwa nyumbani, bango kubwa na linaloonekana wazi lenye maneno “Mpira wa Miguu Unaunganisha Dunia, Hapana kwa Ubaguzi” pamoja na nembo ya Shirikisho la Soka la Israel. 

Ukubwa, mpangilio na mahali pa kuwekwa kwa bango hilo uwanjani vitawasilishwa kwa FIFA angalau siku kumi na tano (15) kabla ya kila mechi kwa ajili ya kuidhinishwa.

Ndani ya siku sitini baada ya kupokea taarifa ya uamuzi huu, Shirikisho la Soka la Israel litapaswa kutumia  theluthi moja ya faini iliyotajwa katika kutekeleza mpango wa kina wa kuhakikisha inachukua hatua dhidi ya ubaguzi na kuzuia matukio kama hayo yasijirudie, kwa kuzingatia kifungu cha 15 aya ya 7 ya Kanuni ya Nidhamu ya FIFA. 

Mpango huo utaidhinishwa na FIFA na utalenga maeneo ya mageuzi, taratibu, ufuatiliaji, na kampeni za elimu katika viwanja na kwenye majukwaa rasmi kwa msimu mzima. 

Kiasi kilichobaki cha faini kitalipwa ndani ya siku 30 tangu kupokea taarifa ya uamuzi.

Kamati imesisitiza tena kwamba ingawa mamlaka yake yamejikita katika utekelezaji wa mfumo wa kanuni za ndani za FIFA, haiwezi kupuuza muktadha mpana wa kibinadamu ambamo mpira wa miguu unafanyika. 

Kwa mujibu wa FIFA, mchezo wa soka unapaswa kubaki kuwa jukwaa la amani, mazungumzo na heshima ya pande zote. 

Uenezi wake wa kimataifa na uwezo wake wa kuunganisha watu unakuja na wajibu wa kulinda maadili ya utu, usawa na ubinadamu, hasa katika nyakati za migogoro na mgawanyiko.

IFA imejulishwa kuhusu sababu za uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya FIFA. Kwa mujibu wa masharti husika ya Kanuni ya Nidhamu ya FIFA, uamuzi huo umechapishwa kwenye tovuti ya FIFA.

Uamuzi huu bado unaweza kukatiwa rufaa mbele ya Kamati ya Rufaa ya FIFA.