Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali Simba, Berkane yanukia kwa Mkapa

Muktasari:

  • Simba imetinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitupa nje Stellenbosch ya Afrika Kusini wakati huo RS Berkane ikiitoa CS Constantine kwenye nusu fainali.

Kama agizo la serikali litafanyiwa kazi kwa wakati, mechi ya marudiano ya hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Simba na RS Berkane itapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Mei 25, 2025.

Hiyo ni baada ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu ‘Mwana FA’ kumuagiza mkandarasi anayesimamia ukarabati wa uwanja huo kuhakikisha maeneo muhimu ya uwanja huo yanakamilika ifikapo Mei 10, 2025.

Mwana FA ametoa maagizo hayo leo, Aprili 29, 2025 katika ziara yake aliyofanya katika uwanja huo.

Katika ziara hiyo, ametoa maelekezo ya ukarabati wa miundombinu mingine muhimu ndani ya uwanja huo, ikiwemo kukamilisha sehemu ya benchi la ufundi la waamuzi kwa kuweka mataili, kuweka viti vya muda katika sehemu zilizo wazi, na kuhakikisha ifikapo ljumaa

kazi hizo ziwe zimemalizika.


Naibu waziri Mwinjuma amesema Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan imetoa maelekezo maalum kuhakikisha Watanzania wanashuhudia historia ya kipekee, kwani mara ya mwisho fainali ya Kombe la Shirikisho kuchezwa Tanzania ilikuwa ni mwaka 2023 ambapo Yanga SC walicheza fainali, na kabla yake mwaka 1993 Simba walifika hatua hiyo.

Mwaka huu, fainali hiyo itachezwa tena nchini na Simba watakuwa wenyeji wa mchezo wa marudiano Mei 25, baada ya kuanza ugenini Mei 17.

"Tunataka Watanzania wajivunie, wajione sehemu ya historia. Kombe linakuja hapa nyumbani na tunataka uwanja huu uwe tayari kulipokea," amesema Mwana FA.

Simba imeingia hatua ya fainali baada ya kuitoa Stellenbosch FC ya Afrika Kusini kwa bao 1-0 katika mechi mbili baina yao.

Katika fainali, Simba itaanzia ugenini dhidi ya RS Berkane, Mei 17, 2025 na mechi ya marudiano itakuwa hapa nyumbani Mei 25, 2025.