Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dube alamba dili jipya Azam FC

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyemaliza na mabao 11 kwenye Ligi Kuu Bara msimu ulioisha, tayari viongozi wa Azam wamempa dili hilo baada ya mkataba wake kubakia mwaka mmoja ambao ungemalizika 2024.

KLABU ya Azam FC imeshtukia jambo na kuamua kumuongezea mkataba mshambuliaji wa timu hiyo Mzimbabwe, Prince Dube utakaomuweka kwenye viunga vya Chamazi hadi mwaka 2026.

Nyota huyo aliyemaliza na mabao 11 kwenye Ligi Kuu Bara msimu ulioisha, tayari viongozi wa Azam wamempa dili hilo baada ya mkataba wake kubakia mwaka mmoja ambao ungemalizika 2024.

Akizungumza na Mwanaspoti jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Abdulkarim Amin 'Popat' alisema mchezaji huyo amekuwa muhimu kwenye kikosi hicho hivyo wasingetamani kuona anaondoka kirahisi.

"Tuko kwenye wakati wa kuboresha timu kwa maana ya usajili mpya lakini wakati tukifanya hayo tunaendelea kuongezea mikataba mipya kwa wachezaji tunaoona watakuwa na msaada mkubwa kwa ajili ya msimu ujao," alisema.

Dube alijiunga na Azam FC Agosti 2020 akitokea timu ya Highlanders ya nchini kwao ambapo katika misimu mitatu aliyoichezea amefunga jumla ya mabao 27 kwenye Ligi Kuu Bara.

Mbali na Dube mastaa wengine walioongezewa mikataba mipya ni Idris Mbombo, Nathaniel Chilambo, Lusajo Mwaikenda, Abdallah Kheri 'Sebo', Malickou Ndoye, Daniel Amoah, James Akaminko na Sospeter Bajana aliyekuwa anawindwa na Simba.