Droo ya mchujo Mabingwa Ulaya leo mchana
Muktasari:
- Timu nane tayari zimeshafuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambazo ni Arsenal, Liverpool, Chelsea, Bayern Munich, Tottenham Hotspur, Barcelona, Sporting na Man City.
Dar es Salaam. Droo ya mechi za mchujo za Ligi ya Mabingwa Ulaya kuwania nafasi nane za kucheza hatua ya 16 bora inatarajiwa kufanyika leo kuanzia saa 8:00 mchana kwa muda wa Tanzania.
Tukio hilo limepangwa kufanyika jijini Nyon, Switzerland katika Makao Makuu ya Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA).
Katika droo hiyo, timu ambazo zinatoka nchi moja zinaweza kupangwa kukutana kama ambavyo pia timu zilizokutana katika hatua ya ligi ya mashindano hayo zinazvyoweza kupangwa kukutana tena.
Timu zinazohusika katika droo hiyo ni 16 ambazo zimeshika nafasi ya tisa hadi ya 24 ndizo zitashiriki katika droo hiyo ambapo zilizoshika nafasi ya tisa hadi ya 16 kwenye hatua ya ligi zitawekwa katika chungu kimoja na zile zilizomaliza katika nafasi ya 17 hadi ya 24 zitakuwa katika chungu kingine ambapo kila timu ya chungu kimoja itapangwa kukutana na mpinzani kutoka chungu kingine.
Kwa mujibu wa utaratibu wa mashindano hayo, timu zilizomaliza katika nafasi ya tisa hadi ya 16 zitaanzia mechi zao za hatua ya mchujo ugenini na kumalizia nyumbani.
Mechi za kwanza za hatua ya mchujo zitachezwa Februari 17 na 18 mwaka huu na za marudiano zitakuwa Februari 24 na 25 mwaka huu pia.
Timu nane ambazo zitaanzia ugenini na kumalizia hatua ya mchujo nyumbani ni Real Madrid, Inter Milan, PSG, Atalanta, Bayer Leverkusen, Juventus, Newcastle United na Atletico Madrid.
Ambazo zitaanzia nyumbani na kumalizia ugenini ni Borussia Dortmund, Olympiacos, Clube Brugge, Galatasaray, Monaco, Qarabag, Bodø/Glimt na Benfica.
Klabu nane ambazo tayari zimeshafuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambazo ni Arsenal, Liverpool, Chelsea, Bayern Munich, Tottenham Hotspur, Barcelona, Sporting na Man City.