Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dani Alves hataonekana Russia

Muktasari:

  • Alves anaungana na wachezaji wengine wa mataifa tofauti ambao wameumia wakati huu makocha wa timu hizo wakijiandaa kuita wachezaji kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa itakayofanyika nchini Russia kuanzia Juni 14 mwaka huu.

Dodoma: Baada ya kushuhudiwa beki wa kutumainiwa wa Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa, Laurent Coscielny akikosa Fainali za Kombe la Dunia kutokana na kuumia wakati wa mchezo wao wa nusu fainali wa Kombe la Europa League wiki iliyopita, Mbrazil Dani Alves naye hatashiriki.

Alves anaungana na wachezaji wengine wa mataifa tofauti ambao wameumia wakati huu makocha wa timu hizo wakijiandaa kuita wachezaji kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa itakayofanyika nchini Russia kuanzia Juni 14 mwaka huu.

Alves beki wa kulia wa klabu ya  PSG ya nchini Ufaransa aliumia kifundo cha mguu alipokuwa anaitumikia klabu yake PSG iliposhinda kwa Les Herbiers mabao 2-0 Jumanne iliyopita.

Chama Cha Soka Brazil  (CBF) tayari kimethibitisha mchezaji huyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu yao ya Taifa itakayokwenda Russia.