Clara Luvanga akitamani kiatu Saudia

Nyota wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga Al Nassr ya Saudia, Clara Luvanga amesema anatamani kuchukua kiatu cha mfungaji bora msimu ujao wa mshindano nchini humo.
Msimu uliopita straika huyo alimaliza na mabao 11 akiwa kwenye nne bora za wafungaji mbele ya Ibtissam Jraidi wa Al Ahli aliyefunga mabao 17.
Akizungumza na Mwananchi, Clara alisema malengo yake makubwa msimu huu ni kuisaidia timu hiyo kutetea ubingwa wa ligi kisha kuchukua kiatu cha ufungaji.
Alisema msimu uliopita alikosa kiatu kwenye mechi za mwisho ambazo ziliamua kiatu kwenda kwa Ibtissam wa Ahli.
"Msimu uliopita nilikuwa bora natamani huu uwe zaidi ya uliopita, naamini nitafunga mabao mengi zaidi niisaidie timu yangu na niibuke mfungaji bora," amesema Clara
Msimu huu tayari timu hiyo imecheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya PFC Femenino ya Hispania, Nassr ikiibuka na ushindi wa mabao 7-2 huku Clara akiweka kambani mabao matano.