Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Novatus atua Uturuki, ajifungia Goztepe

Muktasari:

  • Kiungo Novatus Dismas amejiunga na Goztepe ya Uturuki kwa mkataba wa miaka minne, akitokea Zulte Waregem ya Ubelgiji.

Dar es Salaam. Goztepe inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki leo imekamilisha uhamisho wa kiungo kiraka wa Tanzania, Novatus Dismas kutokea Zulte Waregem ya Ubelgiji.

Kiungo huyo ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika timu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine, anajiunga na Goztepe kwa mkataba wa miaka minne.

“Tunafuraha kutangaza kumsainisha Novatus Miroshi, mkataba wa miaka minne,” ilisema taarifa ya Goztepe.

Novatua anaondoka Zulte akiwa ameitumikia kwa miaka miwili tu tangu alipojiunga nayo mwaka 2022 akitokea Maccabi Tel Aviv ya Israel ingawa aliichezea kwa msimu mmoja tu wa 2022/2023 huku mwingine akicheza kwa mkopo Shakhtar.

Licha ya kuwa na mwanzo mzuri, maisha ya Novatus Dismas ndani ya Shakhtar yalikuwa magumu kutokana na nafasi ndogo ya kucheza aliyoipata hadi alipomaliza mkataba wake wa mkopo.

Dismas ambaye anamudu vyema kucheza nafasi ya kiungo mkabaji na beki wa kushoto, aliichezea Shakhtar idadi ya mechi sita tu msimu uliomalizika huku mbili tu akicheza kwa dakika 90.

Mechi nne kati ya hizo nane ni za Ligi Kuu ya Ukraine, moja ya ligi ya mabingww Ulaya na nyingine moja ya Kombe la Ukraine.

Goztepe itashiriki Ligi Kuu ya Uturuki msimu ujao baada ya kupanda daraja kufuatia kumaliza katika nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza Uturuki msimu uliomalizika.

Timu hiyo inanolewa na kocha Stanimir Stoilov kutoka Bulgaria mwenye umri wa miaka 57 anayependelea kutumia mfumo wa 4-2-3-1 ambaye anainoa timu hiyo tangu mwaka jana Novemba.