Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea njia nyeupe fainali Conference League

Muktasari:

  • Mchezo wa fainali ya Conference League utafanyika Mei 28 mwaka huu nchini Poland kwenye Uwanja wa Wrocław.

Chelsea imezidi kuikaribia fainali ya Kombe la Conference League baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 ugenini dhidi ya Djurgaarden katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya mashindano hayo uliochezwa kwenye Uwanja wa 3Arena.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Jadon Sancho ambaye alifunga la kwanza katika dakika ya 13 akimalizia pasi ya Enzo Fernandes ambaye pia alitoa pasi ya bao la pili lililofungwa na Noni Madueke katika dakika ya 43.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Chelsea ilitoka kifua mbele kabla ya kurudi katika kipindi cha pili ambapo iliendelea kumiliki mpira na kutengeneza nafasi za mabao.

Baada ya mashambulizi kadhaa kwenye lango la Djurgaarden, Nicolas Jackson alipata nafasi mbili ambazo alizitumia vizuri akifunga mabao mawili katika dakika ya 59 akimalizia pasi ya Cole Palmer na dakika ya 65, akimalizia pasi ya Moises Caicedo.

Bao la kufutia machozi kwa upande wa Djurgaarden lilifungwa na Isak Mulugeta katika dakika ya 68 akimalizia pasi ya Tobias Gulliksen.

Licha ya kulalamikia uwanja kabla ya mchezo, kocha wa Chelsea, Enzo Maresca ameonekana kufurahia ushindi walioupata jana huku akisahau kama uwanja ulikuwa wa nyasi bandia.

"Ulikuwa ni usiku mzuri wa nusu fainali muhimu. Ni matokeo mazuri, lakini tuna kumbukumbu ya mchezo dhidi ya Legia Warsaw, ambapo tulishinda 3-0 ugenini lakini tukapata wakati mgumu kwenye mechi ya nyumbani, hivyo tunahitaji kuwa makini kwenye mechi ya pili," amesema kocha wa Chelsea, Enzo Maresca.

Chelsea itarudiana na Djurgaarden, Mei 8 mwaka huu ambapo itakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Stamford Bridge huku ikiwa na nafasi kubwa ya kwenda fainali kutokana na mtaji mzuri wa mabao waliyonayo.

Mchezo mwingine wa nusu fainali ulifanyika kule Hispania kwenye Uwanja wa Villamarin ambapo ilishuhudiwa wenyeji wa mchezo huo Real Betis wakiondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fiorentina.

Mabao ya Betis yalifungwa na Abde Ezzalzouli katika dakika ya sita akimalizia pasi ya Cedric Bakambu huku bao la pili likifungwa na Antony ambaye aliachia shuti kali lililomshinda kipa wa Fiorentina, David de Gea.

Mchezo unaofuata utafanyika kwenye Uwanja wa Artemio Franchi ambapo Fiorentina itakuwa nyumbani kuikabili Real Betis huku mchezo ukionekana bado mgumu kwani timu zote bado zina nafasi ya kusonga fainali licha ya Betis kuwa mbele kwa maba 2-1.

Mchezo wa fainali ya Conference League utafanyika Mei 28 mwaka huu nchini Poland kwenye Uwanja wa Wrocław ambapo mshindi wa jumla baina ya Chelsea au Djurgaarden atakutana na mshindi wa jumla baina ya Real Betis au Fiorentina.