Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United, Spurs zatanguliza mgumu mmoja fainali

Muktasari:

  • Mchezo wa fainali ya Kombe la Europa utafanyika Mei 21 mwaka huu kwenye dimba la San Mamés, Hispania.

Manchester United na Tottenham zimeonyesha matumaini ya kwenda katika hatua ya fainali ya Kombe la Europa baada ya kupata matokeo mazuri kwenye michezo yao ya kwanza ya nusu fainali iliyochezwa jana Mei Mosi.

Man United iliwashangaza wengi kwa kile ilichokifanya Hispania kwenye uwanja wa San Mamés baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Athletic Bilbao.

Casemiro ndiyo alikuwa wa kwanza kuifungia United bao la kuongoza katika dakika ya 30 akimalizia pasi ya Manuel Urgate.

United iliendelea kufanya mashambulizi kwenye lango la Bilbao hadi dakika ya 37 ilipopata mkwaju wa penati baada ya beki wa Bilbao, Dan Vivian kumchezea rafu mshambuliaji wa Man United Rasmus Højlund kwenye eneo la hatari.

Bruno Fernandes ndiyo alipiga mkwaju wa penati na kuandika bao la pili huku Bilbao wakibaki pungufu baada ya Vivian kuonyeshwa kadi nyekundu.

Kabla ya kwenda mapumziko Bruno Fernandes alifunga bao lingine la tatu akimalizia pasi ya Manuel Urgate katika dakika ya 45.

Kipindi cha pili Man United iliendelea kumiliki mpira na kufanya mashambulizi kadhaa ambayo hayakuzaa matunda huku Bilbao nao wakijaribu kutafuta bao la kufutia machozi bila mafanikio.

Hadi dakika 90 zinamalizika Manchester United ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-0 huku ikiwaacha mashabiki wa Bilbao midomo wazi.

Mchezo unaofuata United itakuwa kwenye uwanja wa Old Trafford, Mei 8 mwaka huu ambapo Bilbao itakuwa na kibarua kigumu cha kupindua matokeo kwani watatakiwa kushinda mabao 4-0 ili wafuzu kwenda fainali.

Mchezo mwingine wa nusu fainali ulichezwa pale England ambapo Tottenham Hotspur ilikuwa nyumbani dhidi ya Bido/Glimt.

Katika mchezo huo Tottenham iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 ikitengeneza njia nzuri ya kwenda fainali kwani katika mchezo unaofuata itaingia uwanjani ikiwa na faida ya mabao mawili.

Mabao ya Tottenham katika mchezo wa jana yalifungwa na Brennan Johnson katika dakika ya kwanza akimalizia pasi ya Richarlison wakati bao la pili likifungwa na James Maddison

Dominic Solanke aliihitimisha ushindi akifunga bao la tatu kwa mkwanja wa penati katika dakika ya 61 huku bao la kufutia machozi la Bodo/Glimt likifungwa na Ulrik Saltnes katika dakika ya 83.

Mchezo wa fainali ya Kombe la Europa utafanyika Mei 21 mwaka huu kwenye dimba la San Mamés, Hispania ambapo mshindi wa jumla kati ya Man United au Bilbao atakutana na mshindi wa jumla kati ya Tottenham au Bodo/Glimt.