Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea, Betis fainali ya rekodi Ulaya

Muktasari:

  • Mara ya mwisho timu hizi zilikutana katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2005-06, ambapo kila timu ilishinda mechi moja.

Wrocław. Leo macho ya wapenzi wa soka duniani yataelekezwa jijini Wrocław, Poland, ambako fainali ya UEFA Conference League kati ya Chelsea kutoka England na Real Betis ya Hispania itafanyika katika Uwanja wa Manispaa ya Wrocław kuanzia saa 4:00 usiku.

Chelsea inaingia katika fainali hii ikiwa na kiu ya kuongeza taji lingine kwenye kabati lao la makombe kwani tayari wamewahi kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili (2012, 2021), UEFA Europa League mara mbili (2013, 2019), na UEFA Super Cup mwaka 1998. Endapo kama Chelsea itashinda leo, itaweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kutwaa mataji yote ya UEFA.

Wachezaji wa kuchungwa kwa upande wa Chelsea ni Cole Palmer, ambaye amekuwa na kiwango bora katika safu ya ushambuliaji akiwa amehusika katika mabao 23 kwenye ligi ya Ligi Kuu England (EPL) msimu huu akifunga 15 na kutoa pasi nane za mwisho anatarajiwa kuhamishia makali hayo katika fainali ya leo licha ya kuwa hana bao katika mashindano haya, wachezaji wengine ni Jadon Sancho, Enzo Fernández, Noni Madueke pamoja na Nicolas Jackson, anayetarajiwa kuongoza safu ya mbele baada ya kuwa nje katika mechi za ligi kutokana na kadi.

Kwa upande wa Real Betis, licha ya kuwa ni mara yao ya kwanza kufika fainali ya michuano ya Ulaya, lakini wameonekana kuwa na kiwango imara kinachoweza kuitishia Chelsea, Kocha Manuel Pellegrini, ambaye aliwahi kuinoa Real Madrid na Manchester City, ameisuka Betis kuwa timu inayocheza soka la kuvutia na lenye ushindani.

Wachezaji wa kuchungwa kwa upande wa Real Betis ni Antony ambaye amesajiliwa kwa mkopo akitokea Man United January mwaka huu, yupo Isco, Pablo Fornals pamoja na Cédric Bakambu ambaye amefunga mabao saba katika michuano hii akishika nafasi ya tatu.

Historia inaonyesha kuwa Chelsea na Real Betis zimekutana mara nne katika mashindano ya Ulaya. Chelsea wameshinda mechi tatu, huku Betis wakishinda mara moja. Mara ya mwisho walikutana ilikuwa katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2005-06, ambapo kila timu ilishinda mechi moja.

Betis ilipenya katika hatua ya fainali baada ya kuitupa nje Fiorentina kwa jumla ya mabao 4-3 kwani ilipata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa nyumbani kisha kupata sare ya 2-2 kwenye mchezo wa ugenini.

Kwa upande wa Chelsea ilitinga fainali kibabe baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 5-1 ikiifunga Djurgårdens katika mechi zote mbili za nyumbani na ugenini ambapo ugenini ilishinda mabao 4-1 kisha ikashinda bao 1-0 ilipokuwa nyumbani.