CAF yapeleka Kombe la Muungano Pemba

Muktasari:
- Simba ndio bingwa mtetezi wa Kombe la Muungano ingawa mwaka huu haitoshiriki kutokana na ushiriki wake kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Zanzibar. Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar(ZFF) limeamua mashindano ya Kombe la Muungano na kuchezwa katika Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Hapo awali, Shirikisho hilo lilitangaza kuwa mashindano ya Kombe la Muungano yataanza rasmi Jumatano, Aprili 23, 2025 katika Uwanja wa New Amaan Complex kabla ya kutoa taarifa hiyo.
Katika taarifa iliyotolewa leo Aprili 21, 2025 na Kaimu Ofisa Habari wa ZFF, Issa Chiwile imesema kuwa ZFF imepokea barua pepe(email) kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) juu ya maelekezo ya kitaalamu ya matumizi ya uwanja huo.
"Uwanja wa New Amaan Complex kwasasa umeingia katika mfumo maalumu na matumizi, taarifa ya CAF imebainisha kuwa uwanja huo haushauriwi kuchezwa kwa mashindano yenye mechi nyingi mfululizo," imesema taarifa hiyo
Hivyo, katika kutekeleza agizo hilo mashindano ya Muungano mwaka huu yatachezwa Gombani kisiwani Pemba.