Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BRAZIL 2104: Suarez amng’ata beki wa Italia, Ivory Coast chali

Beki wa Ugiriki, Sokratis Papastathopoulos (katikati) akiwania mpira na kiungo wa Ivory Coast, Yaya Toure wakati wa mchezo wa mwisho wa Kundi C katika Kombe la Dunia uliozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Castelao, Fortaleza. Ivory Coast ilifungwa 2-1. Picha na AFP

Muktasari:

  • Mshambualiji Georgios Samaras alifunga bao la kwanza kwa Ugiriki, lakini Wilfred Bony aliingia akitokea benchi aliisawazishia Ivory Coast kabla ya Ugiriki kupewa penalti ya utata dakika 90, iliyofungwa na Samaras.

Sao Paulo, Brazil. Mshambuliaji mtukutu wa Uruguay, Luis Suarez ameibua mkasa mwingine katika Kombe la Dunia baada ya kumng’ata begani beki wa  Italia, Giorgio Chiellini waliposhinda 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D, huku Ivory Coast wakitupwa nje ya mashindano na Ugiriki kwa kufungwa 2-1.

Mshambualiji Georgios Samaras alifunga bao la kwanza kwa Ugiriki, lakini Wilfred Bony aliingia akitokea benchi aliisawazishia Ivory Coast kabla ya Ugiriki kupewa penalti ya utata dakika 90, iliyofungwa na Samaras.

Kwa matokeo hayo Ugiriki sasa itacheza na Costa Rica wakati Colombia wataivaa Uruguay kwenye hatua ya mtoano.  Colombia wamemaliza wakiwa vinara wa Kundi C baada ya kuichapa Japan kwa mabao 4-1.

Mapema mshambuliaji Suarez alitoa kali ya mwaka kwa kumrukia begani beki wa Italia Chiellini katika eneo la penalti na kumng’ata meno kabla ya Diego Godin kuifungia Uruguay bao pekee kwa kichwa.

Beki Chiellini alishusha chini jezi yake kumwonyesha mwamuzi alama za meno katika bega lake.

Baada ya tukio hilo, Suarez alianguka chini huku akishika mdomo wake kwa madai ya kupigwa kiwiko beki huyo.  Makamu wa rais wa Fifa, Jim Boyce alisema shirikisho lake litachunguza tukio hilo na kuchukua hatua stahiki.

“Nimelitazama tukio ile mara kadhaa katika televisheni,” alisema Boyce.

“Hakuna ubishi kwamba Luis Suarez ni mchezaji bora, lakini kwa mara nyingine anajiingiza katika matatizo yasiyokuwa ya lazima.

England imeondoka kwa aibu baada ya kulazimishwa sare 0-0 na Costa Rica katika mchezo wake wa mwisho wa Kombe la Dunia.

Katika fainali hizi England imeondoka na pointi moja baada ya kufungwa mechi mbili na kupata sare moja.

Kocha wa Italia, Cesare Prandelli ametangaza kujiuzuru wadhifa wake baada ya timu yake kutolewa katika hatua ya makundi nchini Brazil.