Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern yatwaa ubingwa Ujerumani, Kane akiondoa gundu

Muktasari:

  • Harry Kane, ambaye amejiunga na Bayern msimu uliopita akitokea Tottenham, sasa ameweka historia ya kutwaa Ubingwa wa Ligi kwa mara ya kwanza.

Munich, Ujerumani. Bayern Munich wametangazwa kuwa Mabingwa wa Bundesliga msimu huu baada ya Bayern Leverkusen ambao walikuwa Mabingwa watetezi kushindwa kupata matokeo mazuri dhidi ya Freiburg katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Europa Park.

Bayern wametwaa ubingwa huo mapema hapo jana, Mei 4, 2025 baada ya Leverkusen kulazimishwa sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Freiburg matokeo hayo yakiwafanya washindwe kuwafikia vigogo hao wa Bavaria wakati zikiwa zimesalia mechi mbili kumalizika kwa Ligi hiyo.

Baada ya matokeo hayo, Bayern ambayo inaongoza Ligi ikiwa na pointi 76, sasa haitaweza kufikiwa na Leverkusen ambayo inashika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi nane na hivyo Bayern kutangazwa Mabingwa rasmi msimu huu ikiwa ni kwa mara ya 34 katika Bundesliga.

Hii ni mara ya kwanza kwa kocha Vincent Kompany kushinda taji la Ligi baada ya kuteuliwa kuiongoza timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitoka kushuka daraja na Burnley. Kompany ameiongoza timu hiyo kushinda mechi 23, akipata sare saba na kupoteza mechi mbili hadi kufikia kutwaa taji hilo.

Mshambuliaji wa kimataifa wa England, Harry Kane, ambaye amejiunga na Bayern msimu uliopita akitokea Tottenham, kwa miaka mingi amekuwa akikosa mataji sasa ameweka historia ya kutwaa Ubingwa wa kwanza wa Ligi huku akiwa amefunga mabao 24 hadi sasa akiongoza orodha ya wafungaji wa Bundesliga.

Bayer Leverkusen, walianza msimu huu kama Mabingwa watetezi wanaolitaka tena taji hilo, lakini safari yao haikuwa kama msimu uliopita ambao walimaliza bila kufungwa mchezo wowote kwani mpaka sasa wamefungwa mara mbili sawa na Bayern huku wakitoa sare mara 11 tofauti na Bayern waliopata sare mara saba.

Kocha Xabi Alonso, aliyetwaa taji hilo msimu uliopita huenda akaondoka kwenye timu hiyo msimu ujao kwani tangu msimu uliopita amekuwa akiwindwa na klabu kubwa  Ulaya ikiwemo timu yake ya zamani Real Madrid.

Katika mji wa Munich, shamrashamra za ubingwa zimeanza kuonekana mapema mara baada ya Bayern kutangazwa Mabingwa huku mashabiki wa timu hiyo wakimiminika kwa wingi mitaani kusherehekea.

Bayern watakuwa kwenye Uwanja wa Alianz Arena Mei 10 mwaka huu wakiikaribisha Borusia Monchengladbach katika mchezo wa Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga kabla ya kwenda kwenye Uwanja wa Rhein-Neckar Arena kumaliza mbio za Ligi hiyo na wenyeji Hoffenheim.