Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bacca achekelea rekodi mpya Yanga

Muktasari:

  • Kwa upande wa nahodha wa Yanga, Job alimpongeza Bacca kwa kupachika bao la ushindi ambalo limewapa pointi tatu muhimu na kusema ni mchezaji muhimu sana kikosini kwao.
no

Baada ya kuipa pointi tatu Yanga ugenini dhidi ya Ken Gold, beki Ibrahim Hamad 'Bacca' ameanza tambo baada ya kufunga bao lake la kwanza na klabu hiyo tangu amesajiliwa.

Bacca ambaye anaitumikia Yanga kwa msimu wa tatu sasa tangu alipojiunga nayo akitokea KMKM amefunga bao lake la kwanza kwenye timu hiyo kwa sasa akiwa amelingana na mabeki Bakari Mwamnyeto na Dickson Job wote wanacheza eneo la ulinzi wa kati.

Akizungumza na Mwananchi, beki huyo alisema anafurahi kuipa timu yake pointi tatu muhimu kwenye mechi ambayo ilikuwa mgumu kwao lakini amefurahi kwa kuwa sasa amelingana na wapinzani wake Mwamnyeto na Job ambao awali walikuwa wakimtambia.

"Nina furaha kuipa Yanga pointi tatu, lakini pia nina furaha nimefunga bao chini ya Miguel Gamondi kikosi ambacho kila mchezaji anafunga, walianza nimemaliza nawakumbusha tu.

"Ulikuwa mchezo mgumu kila mchezaji alikuwa anapambana kuhakikisha anaipambania timu iweze kupata pointi tatu muhimu kitu ambacho kwa upande wangu nilifanikiwa nikiifungia timu bao ambalo ni la kwanza tangu nimeanza kuichezea timu hii hivyo ni rekodi kwangu," alisema beki huyo wa Taifa Stars.

Akizungumzia mchezo kwa ujumla, alisema matarajio yao kama wachezaji yalikuwa ni makubwa lakini dakika 90 ziliamua kuwapa pointi tatu na bao moja na wameshasahau  matokeo yaliyopita wanaangalia mchezo unaofuata.

Kwa upande wa nahodha wa Yanga, Job alimpongeza Bacca kwa kupachika bao la ushindi ambalo limewapa pointi tatu muhimu na kusema ni mchezaji muhimu sana kikosini kwao.

"Bacca alitumia vizuri nafasi moja aliyoipata licha ya kutengeneza nafasi nyingi hasa kipindi cha kwanza, bao alilifunga litaongeza morali kwenye timu na kwake pia.

"Uwanja haukuwa rafiki kwetu, ndio maana tumepata matokoe hayo, kikubwa ni pointi tatu, sasa tunarudi kwenye uwanja wetu wa nyumbani tutarekebisha makosa tuliyoyafanya ili tuweze kuwa bora zaidi huko mbele."

Yanga imepata ushindi wa pili katika michezo miwili ya ligi iliyocheza msimu huu na inatarajiwa wikiendi hii kuvaana na KMC.