Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI achekelea dabi, aitaja Yanga

Muktasari:

  • Aziz KI alisema hatua ya Yanga kurudi mchezoni na mechi hiyo kukubalika kupigwa Juni 25 anaona wazi kwamba mabingwa hao watetezi watautea ubingwa huo.

Kiungo wa Wydad Athletic, Stephane Aziz KI amechekelea suluhu ya kurejea kwa mchezo wa dabi uliopangwa kupigwa Juni 25 kati ya timu yake ya zamani Yanga dhidi ya Simba kisha akatabiri ubingwa unakwenda huku.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Marekani, Aziz KI alisema hatua ya kupatikana muafaka wa mchezo huo imemfurahisha akishusha presha kwa timu yake kujiondoa kwenye uwezekano wa kupoteza ubingwa msimu huu.

Aziz KI alisema hatua ya Yanga kurudi mchezoni na mechi hiyo kukubalki kupigwa Juni 25 anaona wazi kwamba mabingwa hao watetezi watautea ubingwa huo.

“Nimesikia kwamba muafaka umepatikana ni habari njema nimefurahia hilo, wakati naondoka kulikuwa na huo wasiwasi wa kuchezwa hiyo, ilikuwa inanitisha nikiona kama mchezo hautapigwa Yanga ingeweza kupoteza ubingwa,” alisema Aziz KI.

“Ubingwa ungeweza kwenda Simba hii isingekuwa nzuri kwangu, uliona namna msimu huu ulivyokuwa na mambo mengi, tulikuwa na kuanguka na kuinuka na tulijituma kurudi mchezoni.

“Kuna wakati niliwaambia wachezaji wenzangu kwamba licha ya mechi ambazo tulipoteza msimu huu na kutupunguza kasi lakini mwisho tulitakiwa kuupigania ubingwa hilo ndio muhimu na sasa naona matumaini.

“Kama Yanga ikicheza hiyo mechi nina uhakika watashinda na itakuwa bingwa sina wasiwasi na ubora wa wachezaji wenzangu wala makocha niliowaacha.”

Aidha Aziz KI aliwataka wachezaji wenzake kupambana kwani mechi hizo tatu zilizosalia hazitakuwa rahisi kwa kuwa wanacheza na timu zinazotaka pia ushindi ili ziake vizuri kwenye ligi.

Alisema pia mchezo dhidi ya Simba ambao utakuwa wa mwisho kwenye ligi utakuwa ni sawa na fainali nyingine kabla ya kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Singida Black Stars mechi itakayopigwa Juni 28 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja visiwani Zanzibar.

“Mchezo dhidi ya Simba hautakuwa rahisi utakuwa mgumu na umeona imekuwa mechi ya mwisho kwa hiyo inahitajika kucheza mechi hizi tatu kwa hesabu kubwa.

Aziz Ki usiku wa jana alitarajiwa kuwepo uwanjani wakati Wydad ilipokuwa ikivaana na Manchester United ya England katika mechi ya fainali za Kombe la Dunia kwa Klabu inatayoendelea Marekani.