Azam, Yanga vita ya mastaa 6, makocha wafunguka
Muktasari:
- Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na pointi 35 huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 27.
Dar es Salaam. Mechi ya Azam na Yanga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kesho Jumapili, Machi 15, 2026 itakutanisha nyota sita ambao wamewahi kuzichezea timu hizo kwa nyakati tofauti.
Baadhi ya wachezaji hao walijiunga na timu mojawapo moja kwa moja kutoka upande wa pili na wengine walijiunga nazo wakitokea klabu nyingine.
Katika kikosi cha Azam, yupo Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye alijiunga na timu hiyo kutoka Yanga mwaka 2023.
Ndani ya kikosi cha Yanga, wapo wachezaji watano ambao wamewahi kuichezea Azam FC kwa miaka tofauti na kisha baadaye wakajiunga na Yanga.
Wachezaji hao ni Farid Musa, Salum Abubakar, Mohamed Hussein, Mudathir Yahya na Prince Dube.
Farid, Dube na Salum Abubakar walijiunga na Yanga kwa uhamisho wa moja kwa moja ambao ulikamilika baada ya mazungumzo baina ya pande hizo Mbuli.
Mudathir yeye alisajiliwa na Yanga akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Azamiezi kadhaa nyuma yake.
Mwingine ni Mohamed Hussein ‘Zimbwe’ aliyepo Katika kikosi cha Yanga hivi sasa. Zimbwe amejiunga na Yanga akitokea Simba lakini amewahi kuchezea kikosi cha vijana cha Azam FC.
Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge amesema kuwa timu yake imejipanga kuhakikisha inapata matokeo mazuri dhidi ya Yanga,
“Kesho tunaenda kucheza. Kuchukua pointi kama kawaida. Hivyo tutacheza mchezo kamili na kuonyesha tunaweza kuwa bora,” alisema Ibenge.
Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves amesema kuwa wanafahamu ugumu wa mechi hiyo na wapo tayari.
"Wachezaji wangu wanatanya vizurı sana, tokea nimeingia Tanzania nimepata sare moja tu Kwa kifupi nina timu nzuri ambayo inaweza kukabiliana na yoyote bila wasiwasi.
Ninaposema Azam ni bora haimaanishi kuwa tunaenda kwa hofu, tunajiamini na tutacheza kwa kujituma na kwa nidhamu kubwa,” amesema Goncalves.