Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC yamtambulisha Ibenge kocha mkuu

Muda mchache baada ya kutambulishwa kuwa kocha mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge ameahidi kufanya makubwa ndani ya kikosi hicho akifurahia kupata nafasi ya uwakilishi kimataifa huku akiitaja Simba na Yanga.

Ibenge ambaye amemaliza mkataba na klabu yale ya zamani Al Hilal ambayo ameipa ubingwa wa ligi msimu huu amesema amefurahi kupata nafasi ya kuinoa Azam FC.

Alisema Tanzania kuna timu nyingi nzuri kama Simba na Yanga lakini na wao wana timu na wapo tayari kukabiriana na ushindabi.

“Kama ligi ya Tanzania ni namba nne kwa ubora basi timu zilizopo zina ushindani mkubwa lakini anaamini amekuja kupamba ili aweze kufikia mafanikio na wao wapo kwenye nafasi ya ushindani,” alisema na kuongeza;

“Simba msimu huu imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho ni namna gani kuna timu bora lakini pia kuna Yanga ambayo imetwaa mataji yote msimu huu nahitaji ushindani mkubwa kutoka kwao nipo tayari kwa ushindani.” 

Ibenge alisema anatambua ana cv kubwa lakini hiyo haitoshi kuipa mataji Azam bila kuwekeza nguvu kwenye kujenga timu bora kilichomleta Tanzania ni kuipambania timu hiyo kutwaa mataji ndani na kimataifa.