Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ayoub Lakred atimkia Morocco

Muktasari:

  • Chanzo cha ndani kutoka Simba kinaeleza kukamilika kwa dili la Lakred limetiki baada ya FUS Rabat  kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili kwa  ajili ya kuitumikia msimu ujao na muda wowote atasepa zake akiachana rasmi na Wekundu wa Msimbazi hao.

Dar es Salaam. Wakati mabosi wa Simba wakiendelea kujadiliana juu ya kumtema kipa Moussa Camara au la, taarifa kutoka klabu hiyo ya Msimbazi zinadokeza kuwa, mabosi hao wamemalizana na kipa Ayoub Lakred ambaye anajiandaa kwenda kujiunga na klabu ya FUS Rabat ya Morocco anakotokea.

Kipa huyo, aliyekuwa kipa namba misimu miwili iliyopita kabla ya kuumia na kuletwa kwa Camara, alikuwa akiendelea kulipwa na klabu hiyo licha ya kutotumika kabisa katika msimu huu uliomalizika hivi karibuni na inaelezwa hesabu za kumbakisha zimeshindikana baada ya kupata ofa Morocco.

Lakred alikaa nje ya kazi kwa muda mrefu baada ya kupata majeraha wakati wa maandalizi ya msimu uliyoisha ambapo Simba ilikwenda kupiga kambi nchini Misri, hivyo akasajiliwa Camara aliyemaliza msimu  akiwa kinara  wa cleansheets 19.

Chanzo cha ndani kutoka Simba kinaeleza kukamilika kwa dili la Lakred limetiki baada ya FUS Rabat  kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili kwa  ajili ya kuitumikia msimu ujao na muda wowote atasepa zake akiachana rasmi na Wekundu wa Msimbazi hao.

"Lakred ni kipa mzuri changamoto ilikuwa ni majeraha aliyopata wakati wa maandalizi ya msimu uliyoisha, Simba ilikuwa na majukumu makubwa mbele yake ndiy maana akasajiliwa Camara, ikumbukwe kipindi hicho Aishi Manula naye alikuwa naye majeruhi, hivyo kimataifa ingekuwa ngumu kusalia na Ally Salim na Hussein Abel," kilisema chanzo hicho na kuongeza;

"Simba ilikuwa inataka kumbakiza Lakred lakini inalazimika kufumua kikosi, siku za usoni itakuwa inatoa mkono wa baibai kwa wachezaji wengi, lengo ni kujipanga kikamilifu msimu ujao ili kurejesha heshima ya kunyakua Mataji ya Ligi Kuu na ikiwezekana na CAF."

Mbali na Lakred, kiungo mkabaji Fabrice Ngoma pia inaeleza anajiandaa kujiunga na Hassania Union Sports Agadir pia ya Morocco, baada ya Simba kutoonyesha nia ya kuendelea naye msimu ujao.

Ngoma msimu uliyoisha ameifungia Simba mabao manne, uongozi wa klabu hiyo tayari ulishaanza kusaka mbadala wake wa kuvaa jezi namba sita.

Mbali na hilo pia kuna uwezekano viongozi wa Simba wakaachana na Camara na ulishaanza kusaka kipa mwingine wa kigeni.