Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manula arejeshwa Taifa Stars akinusa rekodi CHAN

Muktasari:

  • Fainali za CHAN 2024 zitafanyika kuanzia Agosti 2 hadi 30 mwaka huu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Dar es Salaam. Baada ya kutojumuishwa katika kikosi kwa siku 221, kipa Aishi Manula ameitwa katika kikosi cha wachezaji 27 wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kitakachoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 siku 37 zijazo.

Fainali hizo za CHAN 2024 ambazo zitafanyika katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania ambazo zimeandaa kwa pamoja zitaanza Agosti 2 na kufikia tamati Agosti 30 mwaka huu.

Tangu Aishi Manula alipocheza mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 dhidi ya Guinea, Novemba 19, 2024, hakuitwa tena katika kikosi cha Taifa Stars kwa awamu mbili tofauti.

Na licha ya kutopata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba, kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ ameamua kuwa naye katika kikosi cha CHAN 2024 huku akimuweka kando Ałły Salim ambaye naye anachezea Simba kama ilivyo kwa Aishi Manula.

Kocha Morocco ameita kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji wazoefu na vijana ambao wanaonekana wamejumuishwa kundini ili wapate uzoefu.

Timu za Simba, Yanga na Azam FC zimetawala kikosi cha Taifa Stars kwa idadi kubwa ya wachezaji wao kuwemo kundini kama ilivyo kwa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’.

Wachezaji 27 walioitwa katika kikosi cha Taifa Stars ni Manula, Hussein Masalanga, Yakoub Suleiman, Shomari Kapombe, Lusajo Mwaikenda, Mohamed Hussein, Paschal Msindo, Ibrahim Hamad na Dickson Job.

Wengine ni Wilson Nangu, Abdulrazack Hamza, Vedastus Masinde, Lameck Lawi, Ahmed Pipino, Mudathir Yahya, Yusuph Kagoma, Nassor Saadun na Kibu Denis.

Pia kuna Jammy Simba, Iddy Selemani, Sabry Kondo, Feisal Salum, Sheikhan Khamis, Clement Mzize, Mishamo Michael, Ibrahim Hamad na Abdul Suleiman.