Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yatema wanne, Partey anabaki

London, England. Klabu ya Arsenal imetangaza kuachana na wachezaji wanne wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo, huku Thomas Partey akianza mazungumzo ya mkataba mpya.

Klabu mbalimbali kutoka Ligi Kuu England zimeanza kufanya usajili kabambe kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu lakini hadi sasa Arsenal bado haijatangaza mchezaji yoyote.

Arsenal imetangaza kuachana na wachezaji wake 20 mwishoni mwa mwezi huu lakini ni wanne tu kati yao ambao walikuwa wakitumika kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Partey ambaye amemaliza mkataba na timu hiyo, anatarajiwa kupewa mwingine wa mwaka mmoja kutokana na umri wake wa miaka 31, ambao utamweka klabu hapo hadi mwishoni mwa msimu ujao.

Kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiyo ilisema kuwa: "Wachezaji wafuatao Chloe Kelly, Thomas Partey, Michal Rosiak mazungumzo mikataba yao inamalizika mwishoni mwa mwezi huu. Mazungumzo yanaendelea na tutatoa taarifa rasmi.

Klabu hiyo imesema kuwa kati ya wale 20 ambao wataachana na klabu hiyo ni pamoja na Raheem Sterling, Kieran Tierney, Neto na Jorginho.

Taarifa hiyo ikifafanua kuhusu kuondoka kwa Sterling ilisema kuwa mkataba wa mkopo wa mchezaji huyo umemaliza.

Jumla ya wanaotarajiwa kuondoka ni  'Nathan Butler-Oyedeji, Reece Clairmont, Khayon Edwards, Jakai Fisher, Romari Forde, Teyah Goldie, Jimi Gower, Jack Henry-Francis, Lina Hurtig, Amanda Ilestedt, Jorginho, Max Kuczynski, Salah-Eddine Oulad M’Hand, Ismail Oulad M’Hand, Neto, Brian Okonkwo, Elian Quesada-Thorn, Zacariah Shuaib, Raheem Sterling na Kieran Tierney'.