Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yashusha mashine ya kwanza

Muktasari:

  • Hata hivyo, inaelezwa kuwa muda wowote kuanzia sasa Arsenal inaweza kukamilisha dili la mshambuliaji wa Sporting Lisbon Viktor Gyokeres, ambaye wameshakubaliana naye kila kitu na kilichobaki ni kusaini tu.

London, England. Arsenal imetangaza kumsajili kiungo wa Real Sociedad, Martin Zubimendi kwa kitita cha pauni 51 milioni ukiwa ni usajili wake wa kwanza kwenye dirisha hili.

Zubimendi, 26, ambaye amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwindwa na Arsenal amesaini mkataba wa miaka mitano.

Awali timu za Liverpool na Manchester United na Man City zilikuwa zinapewa nafasi kubwa ya kumsajili kiungo huyo matata lakini Arsenal ndiyo imeshinda vita hiyo.

Kiungo huyo raia wa Hispania amewahi kusema kuwa anatamani kuitumikia Arsenal na sasa ndoto yake imetimia.

Zubimendi ambaye amepewa jezi namba 36, anakwenda kuziba pengo la Thomas Partey ambaye anaachana na timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika.

Akiwa La Liga kiungo huyo alifanikiwa kucheza michezo 180 kwenye timu yake ya Real Sociedad, lakini akiwa amecheza mechi 18 tu kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania.

 "Hii ni hatua kubwa kwenye maisha yangu ya soka, hili ni jambo ambalo nilitamani litokee miaka mingi iliyopita, lakini ni rasmi kubwa limekuja wakati muafaka sana. Nilipoingia hapa ndiyo nimefahamu ukubwa wa klabu hii.

"Nimefurahishwa na Arsenal kwa kuwa staili yao ya kucheza ndiyo ninayoitaka na kuipenda, tukutane msimu ujao," alisema kiungo huyo baada ya kusaini.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa muda wowote kuanzia sasa Arsenal inaweza kukamilisha dili la mshambuliaji wa Sporting Lisbon Viktor Gyokeres, ambaye wameshakubaliana naye kila kitu na kilichobaki ni kusaini tu