Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Al Ahly yaaga ikizoa mabilioni Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Bingwa wa Mashindano ya Kombe la Dunia la Klabu 2025 anapata kitita cha Doła 40 milioni (Sh107 bilioni).

Katika mechi iliyochezwa kuanzia saa 10:00 alfajiri ya kuamkia leo Jumannne Juni 24, 2025 kwa muda wa Afrika Mashariki, wawakilishi wa Afrika, Al Ahly wameaga mashindano ya Kombe la Dunia la Klabu baada ya kutoka sare ya mabao 4-4 na Porto.

Ahly imekuwa timu ya pili ya Afrika kutupwa nje ya mashindano hayo ikifuata nyayo za Wydad Casablanca ya Morocco na sasa matumaini ya Afrika yamebaki kwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Esperance ya Tunisia.

Hata hivyo pamoja na kutolewa, akaunti za benki za klabu hiyo ya Misri zimenona kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ilichovuna katika mashindano hayo yanayoendelea huko Marekani.

Al Ahly imevuna kiasi cha Doła 11.55 milioni (Sh31 bilioni) ambazo zimetokana na mgawo wa kushiriki mashindano hayo na pia kupata matokeo ya sare katika mechi mbili kati ya tatu za kundi lake A lililo pia na timu za Palmeiras, Porto na Inter Miami.

Kwa kushiriki tu mashindano hayo, Al Ahly imepata kitita cha Doła 9.55 milioni (Sh26 bilioni) na kwa kupata matokeo ya sare katika mechi mbili, imepata kiasi cha Doła 2 milioni (Sh5.4 bilioni).

Ifahamike kwamba katika mashindano hayo, timu unayopata ushindi kwenye mechi, inavuna kiasi cha Doła 2 milioni na inayopata matokeo ya sare inajihakikishia kiasi cha Doła 1 milioni (Sh2.7 bilioni).

Kwenye mechi tatu za mashindano hayo, Al Ahly imetoka suruhu na Inter Miami na sare ya mabao 4-4 na Porto huku ikipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Palmeiras. Bingwa wa mashindano hayo, anapata kiasi cha Doła 40 milioni (Sh107 bilioni).